0 0
Read Time:7 Minute, 50 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

KENYA INAVYOWEWESEKA NA TANZANIA.

Na Thadei Ole Mushi.

Vita kubwa ambayo Kenya hupigana toka zamani ni vita ya kibiashara. Taifa la Kenya ni taifa la kibepari sana na kwa muda mrefu limekuwa likinufaika sana na ujinga wa Tanzania kibiashara.

Twende sawa hapa

  1. Mradi wa SGR.

Kuna watakaojiuliza Reli ya SGR inawahusu nini wakenya? Ni swali zuri Sana na kila anayejiuliza ni haki yake ajiulize.

Kama Kuna kitu kinawasumbua Kenya ni Mradi huu wa SGR. Tukumbuke kuwa issue hapa sio mataruma ya Reli Bali issue kubwa hapa ni bandari zetu Mombasa na Daresalam

Ipo hivi

Kenya ndio wa kwanza kabisa kujenga mradi wa SGR wakishirikiana na Ethiopia kwa kukopa China. Mkopo huo waliokopa China uliziingiza nchi hizi mbili Kenya na Ethiopia kushika number mbili na number tatu kwa nchi zilizokopa Sana China Kutoka Africa. Yaani tukipanga wanaodaiwa fedha nyingi na China Africa basi kenya na Ethiopia zinashika number mbili na number tatu. Ni Mkopo ambao ni mkubwa Sana na kuulipa si kazi ndogo.

Jarida la African Report liliwahi kunukuu mtafiti mmoja aliyeandika kwenye Gazeti la Kenya (Daily Nation) kuwa:-.

“Kenya’s and Ethiopia’s SGR projects impacted significantly the amount of their debt to China and generally their ratio of debt relative to GDP,” researchers wrote in the Daily Nation in December 2019, “As of 2017, Ethiopia and Kenya ranked the second and third highest Chinese debtors on the continent respectively. Their debt relative to GDP has also risen exponentially compared to Tanzania’s.”

Further complicating matters is the fact that, despite accumulating debt and government focus over the past decade, Kenya and Ethiopia’s SGR’s have not delivered what they promised.

Pamoja na kwamba Wana Mkopo mkubwa Sana lakini hawatarajii kuvuna matunda yoyote yale kwenye mradi huo. Hawatarajii kuvuna Kama walivyopanga hapo awali. Yaani mipango yao imevurugika….

Sababu za kutokupata faida

Kutokana na mradi huo kutumia fedha nyingi Sana za Mkopo na ugumu wa kulipa Mkopo wenyewe Bandari ya Mombasa imekuwa si rafiki Tena kupitisha bidhaa kwa nchi za Africa mashariki kutokana na masharti na Kodi walizoweka ili wapate fedha za kulipa Mkopo.

Kutokana na hilo bandari Daresalam Tanzania imeendelea kuwa kivutio kwa nchi za Africa mashariki na Kati. Balaa kubwa zaidi kwa Kenya limekuja kujitokeza kwa Tanzania ilipoanza kujenga SGR yake.

Baada ya Mradi kuanza mataifa ya Burundi, Rwanda, na Congo waliingia mkataba wa Reli hii kufika kwenye nchi zao. Kwa maana hiyo Nchi hizi zitakuwa na access ya Moja kwa Moja kwa njia ya Reli na bandari ya Daresalam. Jiulize bandari ya Mombasa Kenya itabaki inahudumia nchi nchi gani? Bandari yao itamlisha Nani? Kwa hiyo SGR yetu imekuja kuwa ni maziko ya bandari ya Mombasa.

Justification

Baada ya Tanzania kutiliana saini na nchi za Burundi, Rwanda, na Congo kuhusu ujenzi wa SGR Gazeti la nchini Kenya linalojulikana Kama the East Africa liliandika kuwa Kenya imepata pigo kubwa kutokana na makubaliano hayo ya Tanzania na Rwanda, Burundi, na Congo. Fuata Link kusoma walichokiandika.

Blow to Northern Corridor as Tanzania signs deal to link SGR to Burundi, DRC – The East African – https://www.theeastafrican.co.ke/business/Tanzania-signs-mega-sgr-deal-with-burundi-drc/2560-5377324-75ujpd/index.html

Hili Ni Gazeti la Kenya sio la Tanzania katika Hali Kama hii hawawezi kutufurahia sisi kupaa kiuchumi.

Habari hii ilichapishwa pia na jarida la The China Project in Africa. Unaweza pia kusoma kupitia link ifuatayo kujionea kinachoendelea.

  1. Mradi wa Stiglers Gorge.

Huu ni Mradi wa umeme ambao kufikia 2022 tunatarajia uwe umekamilia kabisa.

Mradi huu utatupatia megawatt 2,100 sawa na bwawa la Aswan la Misri ambalo nalo linatoa megawatt hizo 2,100.

Stiglers itakuwa bwawa Namba Mbili Afrika yeye na Aswan kwa pamoja kwa kutoa megawatt nyingi na zinazolingana. Mabwawa Mengine yote yaliyobakia Afrika hayawezi kufikia kiwango hicho Cha Stiglers.. number moja lipo Ethiopia.

Mradi huu Rais Magufuli alipoanza kuugusia kuwa ataujenga utoke kwenye ndoto za Mwalimu Nyerere na kuwa kweli hakuna Taifa ambalo halikupinga.

Mataifa ya Ulaya na kwingineko wote waliionya Tanzania wasijaribu. Sababu kubwa wataharibu mazingira….

Mwandishi Kutoka Kenya anayeishi Lusaka Zambia anayeitwa Mike Mwenda aliandika kwenye jarida la Lifegate Mambo ya ajabu kabisa na hata kumtuhumu Rais wetu. Kisa ni sisi kutaka kutengeneza Mradi wa Stiglers. Fuata link ifuatayo kumsoma Mike Mwenda na shutuma zake.

https://www.lifegate.com/people/lifestyle/stieglers-gorge-dam-tanzania

Linapokuja suala la kiuchumi kwa Dunia ya Sasa ni Vita. Na Kama hutoruhusu akili yako kufanya kazi Basi utajikuta ukiitikia chorus za nyimbo za mabeberu.

Stiglers itatuondoa kabisa kwenye uhaba wa umeme na kutufikisha kwenye Uchumi wa viwanda. Kila Tanzania inapojenga Kiwanda Moja kwa Moja unagusa Uchumi wa Kenya ambao hutegemea Sana soko hapa Tanzania kutokana na sisi kuwa hatuna viwanda. Hii ni Vita…..hata Panadol hatununui Tena Kenya.

Tujiulize Kama Stiglers inaharibu mazingira je viwanda vya mabeberu haviaharibu mazingira?…..

Mwaka 1992 Marekani ulikataa kusaini mkataba wa Kyoto Protocol ambao ulihusu kupunguza viwanda ambavyo vinachangia mabadiliko ya Hali ya hewa.

Unaambiwa mataifa haya ya Magharibi pekee huchangia joto Duniani kwa asilimia 45 ya joto lote. Utafiti uliwahi kufanyika na kuonyesha kuwa Kama mataifa haya ya kibepari yatakubali kupunguza Viwanda vyao Basi Dunia inaweza ku maintain joto la centigrade 18°C.

Sisi kujenga Stiglers tu imekuwa kelele kubwa.

  1. Madini ya Tanzanite.

Mwaka 2014 Nchi za Kenya na India ziliipita kwa mbali Tanzania kwa kusafirisha na kuuza katika soko la dunia, madini ya tanzanite ambayo yanapatikana hapa nchini pekee.

Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini kwa wakati huo , Mhandisi Paul Masanja aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwa mwaka 2013, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito.

Kamishna Masanja alisema mwaka 2013 pekee, Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola 100 milioni za Marekani (Sh173 bilioni) dhidi ya Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni) zilizouzwa na Tanzania.

“Katika kipindi hicho cha mwaka Cha mwaka 2013, India iliuza tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 300 milioni (Sh509 bilioni) kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India,” alisema Masanja.

Mwaka 2016 Marc Nkwame, Mwandishi Tanzania Daily News aliripoti kuwa Kenya iliuza tena madini ya Tanzanite njee ya mipaka yake yenye Thamani ya Dola milioni Mia Moja huku India ikifikia dola milioni 300 na Tanzania ambaye ndiye mwenye machimbo akiuza madini ya Dola million thelathini na nane tu.

JPM akatengeneza Dawa!!

Ujenzi wa ukuta wa MERERANI umekuwa shubiri kwa Kenya na India Kwani sasa wamebaki wakitizama show ya uuzaji wa madini moja kwa moja pale Merereni na Tanzania Sasa ndio inayoongoza kwa uuazaji wa madini haya ndani na nje ya nchi fuatilia link ifuatayo kuona yaliyokuwa yakiendelee kwenye sector ya madini.

https://enactafrica.org/research/trend-reports/efforts-to-curb-tanzanite-smuggling-make-tanzania-shine

Hili lilikuwa pigo kubwa sana kwa Kenya.

  1. Mgogoro wa Loliondo.

Wiki hii toka jumatatu issue kubwa kwenye media ilikuwa ni mgogoro wa Loliondo. Catalyst mkubwa kwenye mgogoro ule ni wenzetu wa Kenya.

Tanzania inaweka mpaka kwenye eneo la KM 1,500 tu la Pori tengefu. KM 2,500 wanaachiwa ndugu zetu wafugaji waendelee na shughuli zao. Sababu ya Serikali kuchukua uamuzi huu ni kulinda hifadhi zetu za wanyama zisipotee.

Ipo hivi…

Eneo linalowekewa mipaka ni muhimu sana kwa hifadhi zetu hasa Serengeti kwa sababu eneo hilo ndilo linalotoa asilimia 48 ya maji yanayoingia Serengeti, Ndio eneo ambalo ni mazalia ya wanyawa, ndio sehemu ambayo wanyama wahamao hupita kutoka Serengeti kwenda Masai Mara Kenya, Pori hili ni Chanzo kikubwa cha Mapato ya Serikali kutokana na uwindaji na Utalii.

Shughuli za watu na ongezeko la Watu kwenye eneo hili ni tishio kwa Usalama wa nchi kwa kuwa Maji yakikauka eneo hili tutaua moja kwa moja Mbuga ya Serengeti, mbuga hii ikifa moja kwa Moja wanyama wote watahamia Masai Mara Kenya ambayo angalau ina sifa sawa na Serengeti…

Cha pili Mifugo mingi inayofugwa Pale Loliondo zaidi ya Asilimia 70 ni ya WaKenya. Ndio maana Serikali imekuja na Mpango wa utambuzi wa mifungo kwa kulete sensa ya mifugo kwa kuivalisha hereni. Hili ni pigo lingine kwa Kenya maana ili ngombe wako asajiliwe lazima mmiliki awe Raia wa Tanzania.

Kwa maana hiyo lazima Mgogoro wa Loliondo waupambe kwa sifa zote mbaya…

Tanzania itenge fedha kwa ajili ya program za Vijana kuwaelimisha na kulitambua taifa lao. Itenge pia kundi maalumu la kuwaandaa vijana wa kuja kukamata madaraka ya nchi. Hofu yangu ni kuwa nchi hii kama tukiwaacha vijana wetu kuwekeza kutafuta Kibunda kwenye kubeti tu tutakuja kulipoteza hili taifa. Vijana wengi wanajua makampuni ya Kubeti kuliko hata mambo ya kiusalama wa taifa lao.

  1. Bomba la Mafuta Uganda hadi Tanga.

Kenya ilikuwa nchi ya Kwanza kufanya Lobbying Bomba la Mafuta kutoka Hoima kuelekezwa Kenya. Baadaye Tanzania ikaingia kwenye kuitafuta Fursa hiyo. Kutokana na Tanzania na Uganda pamoja na Museven kuwa na Mahusiano ya Ki mkakati muda mrefu Museven hakuweza kupindua kwa Tanzania. Akakubali lile bomba la Mafuta kielekezwe Tanga badala ya Lamu Kenya. Hili lilikuwa pigo jingine la KO fuata link kusoma magazeti ya Kenya walichoandika.

Baada ya kukosa Dili hilo tuliona wanafunzi wa Kenya wanaosoma nje ya Nchi wakiandamana kupinga ujenzi wa Bomba hilo kwa madai linaharibu mazingira. Walimfuata hadi Rais wa Ufaransa kuingilia kati bomba hilo lisijengwe.

Hii ni hatari kwa Taifa. Litendee haki taifa lako na Share ili vijana wengi wapate maarifa haya.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
100 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %