
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
OIL AND GAS (SMT-SMZ)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kwa sasa Serikali ipo tayari kuwakaribisha wawekezaji wa Mafuta na Gesi Asilia ili kuendeleza shughuli za utafiti na uchimbaji.
Amesema hayo leo katika hafla ya makabidhiano ya ‘Data’ za utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwa vitalu vya Zanzibar ambayo imefanyika viwanja vya Ikulu Zanzibar baina ya Waziri wa Nishati Mhe. January Yusuf Makamba (SMT) na Waziri wa Uchumi wa Buluu Mhe. Suleiman Masoud Makame (SMZ) walikabidhiana Data hizo ambazo zimehifadhiwa katika mfumo wa kielektroniki, nakala ngumu, sampuli za miamba na kikemikali.
Rais Dk. Mwinyi amesema hatua ya kupokea data hizo ni mwanzo mzuri wa kuongeza jitihada za kukuza sekta ya mafuta na gesi asilia.





