
Anaandika Dr Yahya Msangi
Hakuna kosa kuu linalohatarisha ndoa kama kupoteza uaminifu haswaa kuhusu ngono (infidelity). Ni kisa humu kusameheka ila ukijua namna ya kulikabili ndoa inaweza kusalimika. Kwa waislamu tunaambiwa talaka ikitoka malaika mbinguni wanaguna japo talaka ni ruksa (ikifuata taratibu). Lakini ndoa ya imani yôyote ukiingia infidelity inaweza kusambaratika watoto na wazazi na hâta wanandoa wenyewe wakaumia.
Kusalimika baada ya mmoja kubambwa inategemea wote wawili. Aliyebambwa na aliyemmbamba mwenzie
Tuanze na uliyebambwa.
Ukibambwa epuka haya:
- Kukanusha. Kubali haraka. Eleza ulivyoanza mpaka 40 ilipofika. Toa full mkanda.
- Acha kuendelea na mchepuko . Ukiweza muite umwambie mbele ya mkeo au mumeo picha limeishia hapo.
- Usijitetee sijui shetani, pombe, yéyé ndie alikuanza, n.k. Sema ulipenda kwa roho safii. Acha kudai siijui nikikuona ulikuwa unaninyima. Haisaidii. Itaongeza hasira na kutoaminika kweli unaacha au mwendo mdundo?
- Usiache kujibu maswali – Funguka (open up) unayoulizwa kwa ufasaha hâta kama yana kukera. Usiulizwe uLIKUWA unavaa Kinga uanze “Siku zote” huku ulikuwa huvai. Mwambie Wazi “Kuna Siku peku kuna Siku navaa”. Anakuuliza Ili ajue muende kupima au la. Usimuache ana mashaka hatakusamehe. Mficha taarifa huendelea na uhalifu.
- Usimlazimishe akusamehe fastaa. Mpe muda. Sio kumwambia “tukio dogo la kitambo bado unalo kichwani mie nilishasahau”? Hujasahai Ila hutaki uliyemtendea akukumbushe!
- Usikatae adhabu atakayokupa. Ni Sawa hakimu akusomee hukumu umwambie “sitaki”. Ifanye. Kama mbaya haupiti muda atakuambia “uko huru”. Mkeo au mumeo kakubamba anakwambia “kuanzia Sasa sitaki nikuone na wale walevi Ndiyo walikuponza” unajibu “mie siwezi kuwaacha la sivyo nawe uwaache rafikizo”! Yéyé hajachepuka ukammbamba!
Uliyebambwa ufanye Nini:
- Kudhalilisha
Kuwahusisha wengine hâta Watoto Wenu. Mkabili fargha. Sio unazima redio watoto na majirani wasikie. Mtaa mzima unawasimulia. Unawaslika mashoga Kwenda kumkabili mchepuko wake. Kuchepuka kwa mumeo au mkeo ni aibu shirikishi (collective shame). Wote wawili mnaingia fedheha. - Muonee huruma aka kuwa na “empathy”. Jifikirie ungebambwa wéwé. Usimtizame mwenza kama ibilisi au shetani kibwengo. Kumbuka Sara aliambiwa nini alipochukia mumewe kuchepuka na kijakazi? Bado anaweza kuwa mke au mume bora kwako.
- Usimtake ajirekebishe. Mwachie uamuzi wa kujirekebisha.
- Amini kuwa mwenza kakusaliti. Acha kujihoji “HIVI kweli mama chausiku kachepuka n’a mchoma mkaa”? Hivi baba kolo kachepuka na hausigeli wetu? Kachepuka! Kubali.
- Usikimbilie kufukuza, kuondoka, kutoa au kudai talaka. Huna uhakika atakayefuata hatakuchepukia. Hutupi gari kisa limegonga mtu !
- Usilipe kisasi. An eye for an eye makes everyone blind. Sera ya jiwe kwa jiwe waachie ACT. Mwenza anaweza asikubambe ukabambwa na mtu baki aka mume au mke au mpenzi wa mchepuko wako. Utaingia fedheha kuliko.
- Endeleza huduma kama kawaida. Usiboreshe au kupunguza.Ukiboresha inageuka hongo. Ukipunguza ina maanisha hujasamehe.
- Mweleze jinsi bado unavyompenda na jinsi usivyotamani ndoa ife. Hii itamtibu kisaikolojia. Mtake afikirie watoto wenu ikiwa mtatengana.
- Acha kutumia kosa lake kujinufaisha. Kama héla unaomba ndefu kumkomoa. Kama mechi unataka muda woote utadhani viporo vya bunju ili umkomoe. Akiomba ruksa kwenda kwao unamwambia “umeanza tena”?
Hapa inatosha.
Note: WACHA MAONI YAKO (Comment)








