Tarehe 3 Februari 1969, Majira ya saa4 asubuhi, Dr. Eduardo Mondlane alitoka nje ya Nyumba namba 201, Mtaa wa Nkrumah Dar es Salaam zilipokuwa ofisi za FRELIMO. Akachukua bahasha kadhaa zilizokuwa kwenye sanduku la barua mlangoni hapo kisha akaelekea Osterbay kwa rafiki yake, Mmarekani, aliyeitwa Betty King!
Alizoea kwenda kufanyia kazi hapo, hasa nyakati za asubuhi kuepuka kelele na joto kali la Jiji la Dar es Salaam. Alipofika Osterbay, “Beachfront Villa” alifungua kifurushi kilichokuwa na kitabu cha Georgi Plekhanov!
Alipofungua kitabu kile kilichokuwa na stamps za Moscow alilipukiwa na bomu na kufariki Dunia!

Na
Francis Daudi








