
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
MAMA YANGU SAMIA SULUHU HASSAN BORA UTUMIE MUDA MWINGI KUWATAFUTA WAKINA ANTHONY MTAKA WENGI ZAIDI KULIKO KUWA NA WATU AMBAO WATAKUCHELEWESHA.
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
September 5,2022.
Vijana wengi wa CCM na nje ya CCM kwa sasa akili,macho na masikio yapo kwenye kichwa cha Mama yangu Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mtu pekee kwa sasa mwenye mamlaka ya kikatiba ya kuteua na kutengua nafasi za uteuzi ndani ya Chama na Serikali.
Wapo vijana ambao kwenye mfumo wa Chama na mfumo wa Serikali ambao kwa sasa wanaangaika kule na huku, usiku na mchana kuhakikisha wanaingia au wameingia katika mkeka ujao wa Mama wa MaDC,MaDED na MaDAS,sio kitu kibaya tatizo ni njia zao wanazotumia kuzipata nafasi hizi.”Lobbying”.
Ushauri wangu kwako Mama yangu Samia Suluhu Hassan, ni kwamba wakatae vijana wa namna hii usiku na mchana na wanapaswa kujua kuwa nafasi hizi sio ulaji,nafasi hizi zinaendana na sifa na uwezo.Lazima tujenge nidhamu ya vijana wetu ndani ya Chama sababu kwa kufanya hivyo ndio tutapata wale ambao wataenda kweli kukubeba na kukuvusha uchaguzi wa mwaka 2025 dhidi ya washindani wetu.
Nakumbuka wakati unawaapisha Marc na Maras mwezi jana,Mh Rais uliweka bayana kwamba uteuzi wako uongozwa na vitu vikuu vitatu(I) uwezo,(II)sifa na (III)utiii wa mteule kwa Serikali ya awamu ya sita na ukaendelea kusema kuwa, suala la ukanda au sura ya mtu kwako halina nafasi kabisa kabisa zaidi ukasema kama ntawaletea wateule wabovu basi lawama unazibeba wewe.It was a very fame statement to the Publics.
Kwa maoni yangu natarajia kuwaona wakina “Antony Mtaka” wengi zaidi katika teuzi hizi zijazo kuliko wakati mwingine wowote na sababu zipo wazi kabisa na wewe nadhani unazijua zaidi kuliko Mimi.Serikali yako ya awamu ya sita lazima ijipambanue na Serikali zingine zilizopita kwa wateule wake kuwa ni watu wenye sifa kubwa tatu;
I.Wateule wenye uwezo mkubwa wa kubeba na kuyatetea mbele za watanzania wengine maono,matamanio na dira yako wewe uliowateua na sio vinginevyo.Kamwe tusirudie kufanya makosa ya kubeba wateule ambao hawaamini katika maono,matamanio na dira yako wewe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mwiko.
II.Wateule wenye kiu, maono na uwezo wa juu kabisa binafsi wa ”kubeat” maono na dira yako wewe Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Nakunukuu wewe mwenyewe hapa.
”..kama Mimi Silali,wewe unapata wapi huo usingizi..”.
Kuwapata wateule ambao hawatolala usingizi kwa ajili yako na kwa ajili ya CCM sio kitu rahisi sana,lkn naamini kupitia vyombo vyako na nyavu zako, vijana wa namna hiyo tunao ndani ya Chama na nje ya Chama,tuwatafute mpaka tuwapate.
III.Wateule ambao wanaweza kwenda na kuweza kutafsiri kwa ubunifu,weledi na aggressively Ilani ya uchaguzi wa CCM ya mwaka 2020/2025,mipango mbalimbali ya Maendeleo ya Taifa na mipango yako ya kibajeti ya kila sekta.
DC, DED au DAS ambaye mipango hiyo mitatu haipo kichwani kwake na zaidi hawezi kuitafsiri kwa kuangalia mazingira ya eneo lake,ni wazi anaenda kutuchelewesha kuelekea mwaka 2025.Kwa sasa Rais wangu unahitaji wateule ambao watayapeleka maendeleo katika maeneo yao ya utawala mchakamchaka.
Hatuhitaji tena wateule ambao wewe Mh Rais ndio utakuwa unawapeleka mchakamchaka zaidi ,tunahitaji MaDC, MaDED na MaRAS ambao wataendana na kasi ya CCM ya sasa ya Mzee Abdulaman Kinana, Daniel Chongolo na Shaka Hamdu Shaka.
Haiwezekani tukawa na CCM ya sasa ambayo hailali then tukawa ma wateule ambao wamelala, haiwezekani.
Vijana wenzangu wa CCM tuache kusumbua “wazee” zaidi tuache nafasi hizi zikufwate na sio kuzitafuta kwa udii na uvumba.Utumishi ni mzigo kwa mtu makini na sio fursa.
Mwandishi ni kijana kada wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani , Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini,Mtia nia Ubunge Jimbo la kyela 2020.
+255746726484.