0 0
Read Time:47 Second

WU® MediaPRODUCTION Media

Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji wa Saudia Arabia, Lt. Gen. Suleiman bin Abdulaziz Al-Yahya ametembelea ofisi za Uhamiaji Kurasini siku ya Jumatano Septemba 07, 2020 katika ziara ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano, pia kubadilishana uzoefu wa masuala ya kiuhamiaji pamoja na kuwasilisha rasimu ya mkataba wa ushirikiano utakaosimamia masuala ya ajira kwa watanzania wanaokwenda kufanya kazi katika nchi ya Saudia Arabia kwa maslahi mapana ya nchi hizo mbili.

Kamishna wa Uhamiaji Edmund Mrosso ambaye ndiye aliyepokea ugeni huo, ameeleza kuwa kijiografia Tanzania imekuwa ikipokea wageni kutoka Mataifa mbali mbali ikiwemo Saudi. Hivyo ziara hiyo imeimarisha zaidi mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizo mbili.

Katika ziara hiyo, ugeni huo uliambatana na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Abdullah Ali Al-Shehri pamoja na Mhe. Balozi Hemedi Iddi Mgaza, ambaye ni Mkurugenzi wa Dawati la Masuala ya Uhamiaji kwa Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %