0 0
Read Time:2 Minute, 39 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Mwalimu wao ni India!

Wana Diaspora wa Tanzania wazidi kudadavua kwenye mijadala mizito inayoendelea kwa njia ya kidigitali kuhusu mustakabali mzima wa Hadhi maalumu, Uraia pacha na Nini mchango wao kwa nchi Yao Tanzania. “Je Diaspora Wana mchango Mkubwa kiasi kutokuwepo uraia pacha kunazuia nguvu yao kwenye uwekezaji?”

Baada ya Nigeria, Ethiopia ina diaspora ya pili kwa ukubwa kusini mwa Sahara. Hajifunzi kitu kutoka Nigeria (Diaspora ya hovyo kuliko zote duniani). Inajifunza kutoka India (Diaspora bora duniani). Wameajiri wataalamu wa hadhi maalumu kutoka India.

Sera yao ya diaspora bado wanaiboresha lakini mpaka sasa wamefanisha haya;

1.Ethiopian Origin Identity Card (Yellow Card) Hadhi Maalumu

Hii inawapa diaspora wao (wazawa na vizazi vyao) haki za uraia wa Ethiopia. Ni haki zote isipokuwa kupiga kura, uongozi wa siasa na baadhi ya kazi za serikali kama wizara ya ulinzi, usalama na mambo ya nje.

2. Motisha kwa wanaorudi nyumbani

Wanadiaspora wanaorudi nyumbani waliruhusiwa kuingiza mizigo yao Ethiopia bila ya kodi 100%. Ila hili zoezi lilisimamishwa mwaka 2006 kwa sababu kuna watu waliingiza magari kinyemela. Walitumia majina ya watu wengine.
***Hapa tunaweza kufanya mazungumzo na serikali wanadiaspora tukapunguziwa au kuondolewa kodi na ushuru tunapopeleka mizigo Tanzania ***

3.Motisha kwa wanadiaspora katika uwekezaji nyumbani

Wanadiaspora wao wana haki sawa na wenyeji (wananchi). Hawalipi kodi za uwekezaji na hawagawani faida na serikali.

4. Akaunti za pesa za kigeni

  • Wana fixed akaunti kuanzia miezi mitatu na kuendelea. Kiwango cha kufungulia akaunti ni kuanzia dola 5000.
  • Akaunti za kawaida (checking account) kuanzia dola mia.
  • Akaunti maalumu za savings ambazo zina interest mara mbili ya akaunti za kawaida kwa mujibu wa benki kuu ya Ethiopia.

5.Huduma za utumaji wa pesa

Serikali yao imeweka sheria kwa makampuni ya kutuma pesa na inasimamia reti za utumaji pesa.

6. Diaspora Bond

Hii bondi ni kwa ajili ya kusaidia shirika lao la umeme (EEPCO). Kima cha chini cha hii Bond ni dola 500. Interest ni kati ya asilimia 4 mpaka tano. Na ni kwa muda wa miaka mitano, saba na kumi. Hii bond haina kodi. Inalipwa kila mwaka. Na hii bond inaweza kutumika kama dhamana kwenye kuchukua mikopo benki. Unaweza kusema TANESCO ya Ethiopia inaendeshwa kwa pesa za wanadiaspora wao -kudaaadeki!

7.Programs za elimu na kazi za kitaalamu

Wanadiaspora wenye elimu na ujuzi fulani wanaweza kurudi nyumbani kusaidia kazi kwa kipindi cha miezi sita au zaidi. Wafanyakazi hawa hulipiwa nyumba, nauli za ndege nk.

Tunazungumzia nchi inayorusha ndege zaidi ya mbili kila siku kutoka Marekani kwenda Addis Ababa. Na asilimia zaidi ya sabini ndani ya ndege ni waethiopia. Na bado ndege zao zinaruka duniani kote.

Hawa wanadiaspora wananufaika na nchi yao, wanaisadia nchi yao. Na ni waethiopia watupu. Hawana uraia pacha na hawana mpango nao.

Sisi tuna raia wanazaliwa katikati ya jiji la Dar , mpaka wanakuwa watu wazima kiswahili hawajui na wana paspoti za nje wanazificha. Hawajengi nyumba, wanachukua mikopo benki hawalipi, wako mguu moja ndani, mguu mmoja nje. Kuwapa uraia pacha ni kuhalalisha uharamia wao.

Na wale wa mahakamani, wajifunze kitu hapa. Diaspora bora ni ushirikiano (maridhiano) kati ya wanadiaspora na serikali. Paspoti mbili na viza ya kwenda Kenya ni mtazamo finyu sana wa kuombea uraia pacha. Serikali iliyopelekwa mahakamani inatoaje bonds na akaunti maalumu kwa wanadiaspora?

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %