0 0
Read Time:1 Minute, 23 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Mjadala wa Uraia pacha na Hadhi maalumu waigawa Diaspora.

Kizungumkuti kwa Diaspora wenye Uraia wa nje kwa njia ya ukimbizi

kwa walio jilipua”

HADHI MAALUMU SUPREMACY

Chaguo la wajanja wa ughaibuni!

HADHI MAALUMU inahitaji cheti cha kuzaliwa Tanzania na vitambulisho vya uraia wa nje (paspoti). Visipolingana (kwa waliojilipua na waongo). Hili tatizo litamalizikia uhamiaji ya Tanzania. Kuwa mpole basii, yaishe kindugu. Wanajua umejilipua. Ebo!

Na asikudanganye mtu huko clubhouse kuwa utalipa viza ndani ya Afrika ya mashariki. Kitambulisho cha uhamiaji (hadhi maalumu) utapeta nacho Afrika ya mashariki yote.

URAIA PACHA utahitaji paspoti mbili. Itakuwa ni rahisi kuipata ya Tanzania kwa sababu utatumia cheti chako cha kuzaliwa.

Ila sasa kama ulidanganya umezaliwa Mogadishu au Kigali ili upate paspoti ya ukimbizi, paspoti ya Tanzania itaandikwa umezaliwa Tanzania.

Hata kama hukujilipua. Wanadiaspora waliofoji majina, benki statements, umri nk ni kama asilimia 70 hivi. Uongo wowote uliopo kwenye paspoti yako ya nje, ukishindwa kuurudia kwenye paspoti ya Tanzania wewe ni jipu unasubiri kutumbuka.

Hakikisha paspoti zako mbili zinafukuzana kama tairi la mbele na nyuma. Yakikutana hayo matairi ni ajali.

Maana yake nini? Maana yake ni paspoti zako mbili hizo zikikutana katika deski lolote la airport na zina tofauti ya kimsingi kama nchi uliyozaliwa, kitakachofuata ni Segerea kama ni Bongo. Kama ni nje itakuwa kesi ya ugaidi au kujipatia uraia wa nje kwa fojari. Kama ni mkimbizi wanaweza hata kukudai baga zao za ukimbizi walizokulisha.

Sasa wewe endelea kupandisha sketi juu na kurukaruka “ulaia pacha, ulaia pacha, wakati umesahau kama uliingia Ulaya na Marekani kwa fojari au ukimbizi wa kujilipua.”

Acha kufuata mkumbo. Za kuambiwa ongezea na za kwako.

HADHI MAALUMU WHATSAPP GROUP

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
100 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %