
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Kundi la kwanza ni Diaspora Wanaodai haki ya kuzaliwa hivyo kwao wanaamini kupata Uraia pacha ni lazima kwa kuwa ni haki yao hata kama tayari wameshachukua Uraia wa Nchi nyingine, ambapo wengi wao kwa sasa Wana Uraia wa nje
suala la hadhi Maalumu hawalitaki hata kusikia.
Kundi la pili ni Diaspora ambao wanaamini kuwa kupewa Hadhi maalumu inatosha kwa sababu watakuwa na haki zote kama raia wazawa isipokuwa tu kujihusisha na mambo ya SIASA
Kundi la hadhi Maalumu
hili ni tangazo lao la kuhimiza Diaspora wanaounga mkono Hadhi maalumu kujiunga kwenye makundi sogozi ili kuendeleza harakati
KWA WANADIASPORA WOTE WANAOTAKA HAKI ZA URAIA WA TANZANIA

Kukaa kimya maana yake ni kuunga mkono wanaoenda mahakamani.
Kesi yao haina mshiko wala muelekeo. Na hata wakishinda kimuujiza mahakama haiwezi kubadili sheria wala katiba.
Viongozi wao wanajua hawatapata uraia pacha ila watapiga pesa na wana nafasi ya kutucheleweshea au kufanya tunyimwe hadhi maalumu.
Jiunge nasi tuwe wengi tuwapinge. Hatuhitaji kuibia watu dola elfu 30. Tunahitaji wingi wetu wa kutoa ushuhuda wa kuwashushua mahakamani.
https://chat.whatsapp.com/K4AlLOMv9StHntrjNY4BLR
https://t.me/+Pp6UKcHdfHU5MDVh
KUNDI LA URAIA PACHA

Kundi hili lipo katika mchakato wa kukusanya pesa kiasi Cha dollar 30000$ ili waipeleke serikali MAHAKAMANI , tayari wamesha jipambanua kuhusu watetezi wao yaani mawakili WABOBEZI.








