0 0
Read Time:49 Second

RAIS SAMIA AMEANDIKA HISTORIA UJENZI UWANJA WA MSALATO

Makao makuu Dodoma

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema CCM inapongeza kwa dhati Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwa kuandika historia kwa taifa baada ya miaka kadhaa tangu kuwekwa azimio la makao makuu ya nchi kuhamia mkoani Dodoma.

Shaka ameyasema hayo leo Oktoba 30, 2022 Msalato mkoani Dodoma alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua ni kwa kiasi gani CCM inaridhishwa na utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi baada ya Rais Samia kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato mkoani humo.

“Kama tulivyosikia Oktoba mwaka 1973 ndipo lilipotangazwa azimio la kuhamia hapa Dodoma. Tangu mwaka 1973 hadi leo zimepita awamu mbalimbali na kila awamu ilichukua sehumu ya utekelezaji wa uamuzi huo. Katika awamu hii ya sita ya ndugu Samia Suluhu Hassan kasi ya utekelezaji wa uwamuzi huo imekuwa kubwa sana.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %