0 0
Read Time:2 Minute, 19 Second

WU® MEDIA

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
November 8,2022.

JWTZ ndio chombo pekee Tanzania ambacho kinategemewa sana na Serikali katika kukabili matishio mbalimbali zaidi ya matukio ya vita hasa wakati huu ambapo matishio ya kiusalama,matukio ya ajali na hata natural calamity yanazidi kuibuka siku baada ya siku!

Jeshi la Kisasa lazima liwanze nje ya box na kuondokana na dhana kwamba Military is for War,katika miaka hii Jeshi lazima liwaze katika uwanja mpana zaidi “kuanticipate” matukio ambayo yanaweza kutokea na kuanza kutengeneza programu za mafunzo ya namna hiyo ndani ya Kamandi mbalimbali!

Katika ULIMWENGU huu nilitegemea kila Kamandi ya Jeshi kwa maana ya Air Force Kamandi,Land Force Kamandi na Navy Kamandi wangekuwa na vikosi maalum kwa ajili ya matukio ya Uokoaji kulingana na wings zao au Kamandi zao!Pamoja na kwamba tuna kikosi cha Zimamoto lakini bado Jeshi la Wananchi wa Tanzania, linahitaji sana kuwa na Squad zake maalum za Uokoji Ili kutekeleza kwa vitendo somo letu lile la “AID to Civilian Powers”.

Hiki sio kitu kipya sana duniani,nenda pale UK utakutana na Royal Navy RESCUE team,Land Force Rescue team na Air Force Rescue team.

Mfano,Royal Navy RESCUE Unit ya Nchi ya Uwingereza tayari imeshafanya Operations nyingi na kwa ufanisi mkubwa sana!Mwaka 2000 Op.46, Mwaka 2005 Op.57, Mwaka 2010 Op.59!Inakuwaje mwendesha mtumbwi ndio achukue points wakati wazee mpo?

Sitaki kuamini kuwa pale kwenye Kamandi yetu ya Navy Kigamboni,hatuna wing ya Maritime Search & Rescue team ya maana,sitaki kuamini kuwa team hii haipo ZIWA Nyasa, haipo ZIWA Victoria na haipo ZIWA Tanganyika!

Wakati Majeshi mengi kwa sasa duniani leo tayari yanazungumzia mountain rescue,road rescue,Maritime rescue operations,sisi mpaka leo tunaimba na old form of rescue yaani Kombat Rescue pekee!Haiwezekani!

Leo nimetumiwa sms nyingi sana,wengi wakisema, Uledi wanao”JWTZ”wameshindwa kazi!Unajua why lawama zote zinaenda kwa JWTZ?sababu hiki ndio chombo pekee ambacho Raia wa Nchi hii wanakipa heshima kubwa zaidi!

Sijui nini kilikuwa kinaendelea pale Makao makuu ya Jeshi Upanga”Ngome” baada ya kupata taarifa hii, mpaka tukashindwa kuact kwa haraka zaidi katika tukio la ajali Ile ya ZIWA Victoria”assembling & deployment”.

Nadhani tunahitaji haraka sana kuwaza nje ya box na kutengeneza programu za mafunzo ambazo zinaendana na changamoto zetu za ndani kama Mafuriko,moto na kipunga na vitu kama hivyo!

Jeshini moja ya nilichowahi kufundishwa ni matumizi ya “Initiative” pale ambapo hakuna vifaa vya kutekelezea jukumu fulani liwe la kivita au kiraia!Sikuona initiative yoyote na kwa wakati ya makamanda katika “kucontain” situation Ile,sikuona!

Pole sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Mama Samia Suluhu Hassan,pole sana Makamu wa Rais Mzee Philip Mpango na pole sana Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.Pole sana Spika wa Bunge Mama Tulia Akson Mwansasu!

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %