
WU® MEDIA
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
November 9,2022.
Ni wazi kuwa Profesa Sospeter Muhongo Waziri wa zamani wa Nishati na Madini ana mpango wa kutaka kuivuruga Serikali ya awamu ya sita ya Mama Samia Suluhu Hassan kutokana na michango yake ndani ya Bunge!

Gazeti la Mwananchi la April 09,2022 liliwahi kumnukuu Profesa Muhongo akisema Umeme wa Maji utachelewesha ukuaji wa uchumi wa Tanzania!Badala yake akashauri uwepo wa uchumi wa gesi kwamba ndio unafaa zaidi,aliyosema haya akichangia mpango wa Serikali April 09,2022 Bungeni Jijini Dodoma!
Ni Profesa Sospeter Muhongo huyu huyu aliwahi kuwatangazia watanzania mwaka 2013 kuwa ifikapo Mwaka 2020 Tanzania itakuwa inauza Umeme nje ya Nchi!Mpaka leo Tanzania haijaweza kuwa na Umeme wa uhakika!
Profesa Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini lakini hakuweza kufanya “transition” anayoisema kuhusu Uchumi wa gesi.Profesa pia alikosoa mradi wa BWAWA la Umeme la Mwalimu Nyerere kwamba haupo “visible” kwa Taifa la Tanzania!
January 12,2016 ,Profesa Muhongo huyo huyo alisema Umeme wa Makaa ya Mawe ni WA lazima Nchini na akapendekeza mradi wa Mgodi wa Makaa ya mawe wa Ngaka Wilayani Mbinga,Mkoani Ruvuma!Profesa sijui anasimamia nini!
Repoti za dunia kuhusu Umeme za mwaka 2018 zinasema kuwa Umeme wa Maji ndio Umeme nafuu zaidi duniani!Umeme wa Maji unatumika sana Amerika ya kaskazini sababu Umeme wa Maji kwanza ni (I)Renewable” hivyo kuwa nafuu zaidi,(II) una muda mrefu wa kutoa huduma kwa zaidi ya miaka mpaka 100.

The Centre for Climate Change & Energy Solution” unasema Umeme wa Maji ni nafuu zaidi ambapo Uzalishaji wake ni Senti 2-4 kwa Kilowati kwa lisaa!
Juzi Waziri huyo wa zamani wa Nishati na Madini Profesa Muhongo kupitia mchango wake wa maendeleo ya Taifa unaondelea kuchangiwa Jijini Dodoma na kusema kuwa Tanzania sio Nchi ya Uchumi wa Kati tena!
Kwa mujibu wa recent Publication ya October 20,2022 ya Dkt. Frorence Turuka wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo andiko lenye kichwa “Tanzania Middle Income Country Status & Implications for Future Economic Growth Strategies”.
Andiko hilo la Dkt Frorence Turuka wa Chuo Kikuu cha Sokoine ambaye pia amewahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi,inaitaja Nchi ya Tanzania bado kuwa katika Uchumi wa kati tofauti na mchango wa Profesa Sospeter Muhongo!Pamoja na yote bado Tanzania Ina nafasi ya kurudi kwenye uchumi wa Chini wa kati kabla ya Mwaka 2025 kama kweli kauli ya Profesa Muhongo ina ukweli wowote!
Kwa mujibu wa takwimu na vigezo vya Mwaka 2022 vya kupima nafasi ya Nchi fulani kupima level ya kipato cha Nchini kinasema Nchi ya Uchumi wa chini wa kati”Lower Middle Income Country” ni Dola 1045!Inawezekana ni kweli kuwa kauli ya Profesa Muhongo inaweza kuwa na ukweli fulani lakini bado Tanzania inafanya vizuri zaidi!
Mfano,kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa”TDV” ambayo inabeba malengo makubwa zaidi ya lengo la maisha bora lakini bado Tanzania inafanya vizuri zaidi katika malengo makubwa ya (I)Maisha bora(II)Amani(III) Utulivu (IV)Umoja(V) Utawala bora (VI)Kuwa na jamii ya watu walio na maarifa ya kutosha kufikia Mwaka 2025.(Broad Goals).
Ndani ya mwaka mmoja na nusu wa utawala wa Serikali wa awamu ya Sita ya Mama Samia Suluhu Hassan,Serikali imeweza kutengeneza ajira za kutosha, kupandishwa ngazi ya madaraja kwa Watumishi wa Umma,nyongeza ya mishahara kwa Watumishi wa Umma pamoja na ongezeko kubwa la Bajeti ya kilimo ya Tsh 900+Bilioni.
Ni ngumu sana kwa sasa kumuaminisha Mtanzania wa kawaida kuwa Tanzania imerudi tena katika Nchi ya Uchumi wa chini kabisa kutoka Uchumi wa kati!Huu ni upotoshaji mkubwa kwa Watanzania !
Profesa SOSPETER MUHONGO anapaswa kujihoji kama kweli bado anastahili kuweza kuendelea kuwa Mbunge wa CCM kwa Mwaka 2025 kutokana na upotoshaji wake katika mambo makubwa yenye maslahi kwa Taifa!
Mwandishi ni kijana wa CCM, Makamu wa Rais wa zamani Daruso-IJMC, Ofisa wa zamani Idara ya Habari-Maelezo, Ofisa Kadeti wa zamani Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha, Mhadhiri Msaidizi wa zamani Chuo Kikuu cha Saut na Tumaini na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela Mwaka 2020.
+255746726484.