
Na H.KASHOBA ,Dar Es Salaam
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa tayari amewasili katika Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam kwa ajili ya kufungua Tamasha la Utamaduni baina ya Tanzania na Afrika ya Kusini leo Novemba 18,2022.
Viongozi wengine waliohudhuria ni Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Afrika kusini Mhe. Mcawe Mafu, Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Said Yakubu, Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, pamoja na wananchi mbalimbali wa jiji la Dar es Salaam.
Tamasha hilo litadumu kwa takribani siku kumi ambapo litafanyika katika Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Zanzibar lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo ikiwa ni kutekeleza Mkataba wa ushirikiano katika sekta hizo uliosainiwa mwaka 2011.


