1 0
Read Time:2 Minute, 37 Second

Na Mwandishi wetu NA.

DIASPORA ITALY WASHEREHEKEA MIAKA 61 YA UHURU

Watanzania nchini Italy wamesherehekea miaka 61ya uhuru. Sherehe hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Italia (IN CAMPANIA) zilihudhuriwa na Watanzania kutoka mikoa mbalimbali ya Italy ambao waliziwalilisha Jumuiya zao.

Mgeni Rasmi kwenye madhimisho hayo alikuwa Madame Jubilata Shao (HOC) ambaye alimuwakilisha Mh Mahmuod Thabit Kombo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy, ambaye hakuweza kuhudhuria kutoka na majukumu yake ya Kikazi akiwa nje ya Italy.

from left| Mwenyekiti wa Kamati ya Diaspora Italy Ndugu Kagutta N.Maulidi, ndugu Sigfried Filipo Nnembuka Political and Cultural Councilor. (c) Mh. Jubilata Shao ( HOC) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania (In Campania) Ndugu Judith Joseph, Muambata Fedha Ubalozi wa Tanzania Rome Ndugu Joseph Justine Tarimo

Katika salamu za Mheshiwa Balozi zilizowakilishwa kwa Diaspora na Madame Jubilata Shao, alisema ..”Mh …. Balozi anawatakia heri ya sikukuu ya Uhuru, hata hivyo anasikitika kutokuwa nanyi usiku wa Leo lakini anaamini wawakilishi wake watafikisha salaam zake na kujumuika nanyi katika sherehe za Kumbukumbu Muhimu ya Taifa letu. Mh Balozi anatoa pongezi kwenu na Jumuiya zote kwa kushirikiana kwa Hali na Mali kuandaa na kufanisha sherehe hizi …pia pongezi nyingi kwa Kamati ya Diaspora kwa kusimamia shughuli zote za Jumuiya za Watanzania nchini Italy maana kamati hii ndio mwamvuli wa Jumuiya zote” ….akiwalisha salamu hizi Madame Jubilata alisisiza kwa Wazazi wa Watoto kukumbuka kuwafundisha watoto historia ya nchi ya asili yao TANZANIA.

Sherehe zilinogeshwa Zaidi kwa show ya Msanii wa kizazi kipya Hussein Machozi ambae aliwasha moto wa shangwe mpaka mwisho wa sherehe.

Katika Sherehe hizo mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania In Campania Bi Judith Joseph alitoa tuzo kwa Balozi , tuzo ambayo inashiria kupongeza Mambo mazuri yanayofanywa na Ubalozi kwa kufungua milango ya fursa mbalimbali kwa Diaspora Pamoja na kuwa na mikakati ya kuziunganisha Jumuiya za Watanzania na Diaspora kwa ujumla Kupitia Kamati ya Diaspora. Tuzo pia zilitolewa kwa Kamati ya Diaspora nchini Italy kwa Kazi kubwa ya kuzisimamia Jumuiya za Watanzania nchini Italy. Tuzo pia ilitolewa kwa Dada Eva Nangela Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Genova kwa kuonyesha mfano mzuri kwenye kuchangia kwenye Diplomasia ya Uchumi kwa upandetwa Diaspora kwa kutoa ushawishi Mkubwa kwa wawekezaji na kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya kibiashara na utalii nchini Tanzania.

Tuzo pia ilitolewa Kwa Dada Anna Minja ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Ascoli, kwa kuonyesha ushirikiano Mkubwa Pamoja na utayari wa kuwaunganisha Watanzania wa maeneo Yao.

Pamoja na Mwakilishi wa Balozi kutoka Ubalozi wa Tanzania Rome, Pia alikuwepo Muambata Fedha wa Ubalozi Ndugu Joseph Justine Tarimo. na ndugu SIGFRIED FILIPO NNEMBUKA Political and Cultural Councilor.

Mwenyekiti wa Kamati ya Diaspora wakati akipokea Tuzo kwa niaba ya kamati hiyo, alimuomba mwakilishi wa Balozi,kumfikishia salaam za shukran Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy, Mh Mahamoud Thabit Kombo kwa jitihada zake za kuunganisha Diaspora Nchi Italy Kupitia Kamati ya Diaspora, mwenyekiti pia alimuhakikishia Mh.Balozi kuwa wataendelea kufuata maelekezo yake na kuyafanyia Kazi kwa vitendo na Zaidi Wataendelea KUJIONGEZA.

HOC Madame Jubilata Shao ambaye siku ya Jana alimuwakilisha Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mh Mahamoud Thabit Kombo katika sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika.
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %