Watanzania wanaoishi nje ya nchi (diaspora) wamewekeza Sh2.9 bilioni kwenye Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji (UTT) na Sh2.3 bilioni kwenye mradi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Kigamboni kwa mwaka 2021.

Dar es Salaam. Rais wa Akademia ya Sayansi Tanzania (TAAS), Profesa Yunus Mgaya amesema Serikali imefungua milango ya uwekezaji nchini kwa raia wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi kutokana na mchango wao kwenye maendeleo ya Taifa.








