0 0
Read Time:2 Minute, 39 Second

JICHO LA ULEDI BADO LALIA NA KURUGENZI YA MAWASILIANO

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Desemba 7,2023.

Ni wazi kuwa safari ya kuisimamisha brand yetu na taasisi yetu ya Urais kuanza sasa inaweza kuwa ngumu sana kutokana na aina ya Siasa ambazo zinaenda kutokea kuanzia sasa mpaka mwaka wa Uchaguzi 2025.

Huu ndio wakati mzuri wa kupima uwezo wa watu wetu pale Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu pamoja na Idarani kwa maana ya Idara ya Habari -Maelezo na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali!

Hizi ndio nguzo mbili kuu za kuweza kudetect, kucontain na kucommand game nzima ya political communication ndani ya serikali ya awamu ya Sita!Ni wazi kuwa Chama cha Mapinduzi hasa Idara ya Itikadi na Uenezi ya Chama ndio unayoibeba Mawasiliano ya Serikali kwa sasa!Hakuna ubishi katika hilo!

Mfano,Rais Samia anaonyesha gap la Mawasiliano ndani ya Serikali “..mnaposema tumekopa sana semeni pia kuwa sisi ndio tumejenga sana..”.Hii ina maana gani?hakuna hata mtu mmoja ndani ya Mawasiliano ya Serikali ambaye mpaka sasa katoka na kuifix vizuri hii hoja ya mikopo tunayochukua!

Hatuna mtu ambaye mpaka sasa ndani ya Serikali yangu ambaye kaweza kutoka na kuweza kuiqualify na kuiquantify kisayansi na kujibu hoja ya kwanini tunakopa na implications ya mikopo yetu ni ipi mpaka sasa na matokeo ya baadae ya miradi yetu!

Hii ni moja kati ya hoja ambayo inatawala sana Siasa za mwaka 2023 kuelekea mwaka 2025 hivyo tusipopata watu sahihi wa kuizima uenda ukaleta shida sana huko mbele!Bahati mbaya ajenda ya mikopo ni ajenda ya Siasa za dunia!Nchi ya Sri Lanka inatajwa kuwa Mhanga wa mikopo umiza,Nchi ya Ghana imeingia kwenye msukosuko kutokana na mikopo na juzi Mh Rais wa Kenya, William Rutto katangaza kuikataa mikopo!

Ni wazi kuwa ajenda ya mikopo inaweza kutumiwa vizuri zaidi na wapinzania kwa kucite case studies za maeneo tajwa hapo juu kujustify hoja hiyo kwa hapa kwetu!Sababu ni wazi muwa Serikali yangu ya CCM itaendelea kukopa kwahiyo ni muhimu sana hoja hii lazima iwekwe sawa sasa!

NINI TUFANYE KUANZIA SASA?

I.Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu lazima isukwe kimkakati pia kujibu mahitaji ya Siasa za sasa!Sisemi kwamba Mkurugenzi wa pale atoke,hapana!Pointi yangu ni kuwa kurugenzi inatakiwa kuongezewa nguvu zaidi ya hii sasa!

Hivi nani anamshauri Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu?yupo?Tunahitaji sana mtengenezaji wa mipango ya Mawasiliano awe nyuma ya Bi Zuhura Yunusi!

II.Mkurugezi wa kisasa wa Mawasiliano ya Rais Ikulu lazima awe na elements angalau tatu(i)Communicator(ii)Pursuder au Spin Doctor (iii)na dunia yote iwe kichwani kwake katika kila angle iwe Siasa, Uchumi, Ulinzi na kila kitu!

III.Sioni a clear Coordination kati ya watu wa Mawasiliano ndani ya Serikali na watu wa Mawasiliano ndani ya Chama!Katika siasa za kisasa lazima ajenda ya Mawasiliano ndani ya Serikali ibebane na ajenda ya Mawasiliano ndani ya Chama.Sioni hiyo Coordination kabisa!

Idara ya Habari-Maelezo inawajibika kuwa karibu sana na idara ya Itikadi na Uenezi ya chama tawala and no way the two can work in isolation!Mambo haya yanapaswa kuangaliwa sana sasa !

Wajibu wetu sisi vijana wa CCM ni kushauri tu mengine tunaacha kwa Mamlaka husika!

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %