0 0
Read Time:1 Minute, 6 Second

Na Mwandishi wetu Rome, 12/02/2023

Ujumbe wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pamoja na wajumbe kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar umewasili leo mjini Rome.

46th session of the IFAD Governing Council

The forty-sixth session of the IFAD Governing Council, taking place on 14 and 15 February 2023, will focus on “Accelerating Action for Food Security”.

Ujumbe huo ukiongozwa na mkuu wa msafara Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Mashauri Ndaki,na Waziri kutoka SMZ Mh. Suleiman Masoud Makame wameambatana na Dr. Rashid Tamatama katibu mkuu wizara ya Uvuvi na Mifugo na Dr. Aboud Suleiman Jumbe katibu mkuu Wizara ya Uchumi wa Bluu na uvuvi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Ujumbe huo Mzito umepokelewa Leo tarehe 12/02/2023 na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy, Mh Mahmoud Thabit Kombo.

Tanzania inashiriki kwenye Mkutano wa Baraza kuu la Mfuko wa Maendeleo ya Chakula na Kilimo Duniani IFAD unaotarajiwa kuanza siku ya jumanne tarehe 14/02/2023 Mjini Rome.

Katika mapokezi hayo Mh Balozi Thabit Mahmoud Thabit Kombo alimeongozana na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania akiwemo Mwambata wa KILIMO, Mifugo, Uvuvi na Misitu Bi Jacqueline Mbuya Mhando.

Mh Balozi Mahmoud Thabit Kombo akiwa na Ujumbe wa Tanzania walipokuja kuhudhuria mkutano wa 46th wa IFAD unaoanza Siku ya tarehe 14-15 February 2023

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %