0 0
Read Time:18 Minute, 38 Second

Kutetea Ndoa za Jinsia Moja ni Kukiuka Sheria za Haki za Binadamu za Kimataifa

Na
Obadia Kajungu, Esq.
(ADVOCATE)

Mtandao wa Ushoga Duniani (LGBTQ Movement) ambao unatetea haki za watu wa jinsia moja kuingiliana kimapenzi na kwenda mbali kuhalalisha ndoa za jinsia moja, ni wanaharakati ambao wanapambana kuhalalisha vitendo ambavyo, katika Sheria za Kimataifa havitambuliki.

Serikali kuendelea kutunga sheria za kuhalalisha vitendo hivyo ni kukiuka haki za msingi za binadamu na zinatakiwa kushatkiwa kuulipa fidia ulimwengu wote!

Mtandao huu unadaiwa kuwa ni makundi ya wahuni wenye nguvu kifedha yanayoisumbua dunia kupitia wanasiasa, wanasheria na waandishi wa habari kwa kigezo cha Uhuru wa Kujieleza na Uhuru Binafsi.

Lengo lao ni kuzishinikiza serikali kuhalalisha vitendo hivyo katika sheria za nchi husika.

Mtandao huu tayari umeshayateka mataifa ya mgharibi, hasa Ulaya na Amerika ya Kasikazini.

Kwa upande wa Afrika na maeneo mengine ya dunia mtandao huu unazidi kuzisonga nchi za mabara haya huku ukisaidiwa sana na mataifa yenye nguvu ambayo tayari yameshahalalisha tabia hizi.

Ieleweke kwamba ushoga siyo sehemu ya haki za msingi za binadamu (Basic Human Rights), kama zilivyoainishwa katika Universal Declaration of Human Rights, 1948.

Haki za Msingi za Binadamu (Basic Human Rights) ni zile haki ambazo kila binadamu anazaliwa nazo, yaani “innate rights”. Hizi ni haki ambazo wakati mwingine zinaitwa inalienable rights yaani haki ambazo hazitegemei mazingira aliyozaliwa mtu, malezi aliyolelewa au tabia alizojifunza. Mfano wa haki hizi ni kama vile haki ya kuishi, haki ya kuwa na mahusiano na watu wengine, haki ya kujieleza na kutoa maoni(uhuru wa mawazo), haki ya kuabudu, haki ya kuwa na mali, haki ya unyumba, haki ya elimu, haki ya usiri, n.k.

Hivyo Ushoga kwa sababu mtu hazaliwi nao, siyo haki za msingi za binadamu, bali ni tabia ambazo mtu aidha kwa utundu wake au kuzoezwa na watu wanaomzunguka anajikuta amelemaa kitabia!

Tabia maana yake ni yale matendo ambayo mtu anajikuta amezoea kuyafanya kama sehemu isiyokwepeka ya maisha yake kutokana na mazingira anayoishi au kulelewa au mazoea. Mfano wa tabia ni kama vile ulevi, uzinzi, uvutaji bangi, umalaya, ushoga, wizi, uwongo, ubakaji, n.k.

Nadharia za kisheria zinasema kwamba tabia fulani-fulani za mwanadamu ni lazima zizuiwe ili kuweza kuweka mahusiano mazuri kati ya mtu na mtu au mtu na jamii au mtu na dola au mtu na serikali au mtu na taasisi. Tabia zilizozuiwa na serikali zinaitwa jinai (crimes) wakati tabia zilizozuiwa na dini au jamii zinaitwa maadiili(morals).

Jinai (crimes) maana yake ni tabia ambazo serikali ya nchi fulani imezikataza! Mtu yeyote akivunja sheria za jinai anaadhibiwa kwa kadri ya sheria alizovunja zinavyosema. Kwa mujibu wa Ibara ya 1, na 2 ya Rasimu ya Mkataba juu ya Haki na Wajibu wa Mataifa (Draft Declaration on Rights and Duties of States, 1949) nchi inayo haki ya kutunga na kutekeleza sheria zake bila kuingiliwa na nchi au mtu taasisi yoyote, ili kukidhi mahitaji ya jamii yake zikiwemo sheria za jinai na maadili ya jamii yake. Nchini Tanzania, kitendo cha kufanya ngono kinyume na maumbile ni kosa la jinai na mtu akithibitika kufanya hivyo anaweza kufungwa hadi kifungo cha maisha.

Malengo ya sheria za jinai yanaweza kuwa ni kulinda mali za watu, au uhai, au usalama wa watu wengine, au afya au heshima za watu wengine. Aidha, malengo ya sheria za jinai yanakwenda mbali kulinda uchumi wa nchi, usalama wa nchi kwa upande mmoja lakini pia kulinda maadili, mila, desturi, dini n.k. za jamii na makabila (ethnic societies) dhidi ya tabia au mila au tamaduni za wengine ambazo zitaonekana kuwa na athari za kumeza maadili, mila, desturi, au dini za jamii fulani katika Taifa kwa upande mwingine.

Kwenye Sheria za Kimataifa, Haki za Binadamu zimegawanyika katika makundi makuu mawili ambapo kundi la kwanza linatambua Haki za Kiraia na Kisiasa na kundi la pili linatambua Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni.

Ukiachana na Universal Declaration on Human Rights kuna mikataba mbali mbali ya kimataifa inayohusu au inayogusia Haki za Binadamu kama vile International Labour Organisation(ILO), International Covenant on Civil and Political Rights(ICCPR), Convention on Economic, Social and Cultural Rights(CESCR), African Charter on Human and People’s Rights(AfCHPR), United Nations Convention on Prevention and Punishment of Crimes of Genocide, n.k. Lakini pia kuna Rasimu ya Mkataba kuhusu Haki na Wajibu wa Mataifa (Draft Declaration on the Rights and Duties of States, 1949).

Mikataba yote hii aidha imepitishwa au kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa(United Nations General Assembly).

Ieleweke pia kwamba jamii za Kimataifa hazifanani kimila na desturi au dini hivyo mikataba hii ina masharti maalum kulinda urithi wetu wa kiutamaduni unaojulikana kama “intangible cultural heritage of humanity” wa makabila ya nchi mbali mbali duniani.

Hii ni kwa sababu haipingiki kwamba kuna mataifa kama vile ya bara la Ulaya na Amerika ya Kasikazini hayana makabila kutokana na baadhi ya sababu mbalimbali zikiwemo mapinduzi ya kijamii, kiuchumi pamoja na miingiliano ya watu kutoka pande zote za dunia yamezifanya jamii hizo kupoteza maadili yao, na kujikuta kwamba watu wanaoishi katika jamii hizo ambazo hazina makabila wanalazimika kuvumilia tabia mbaya za majirani zao (social-behavioral tolerance).

Hivyo huwezi ukalazimisha jamii kutoka katika mataifa hayo ya magharibi (Ulaya ya Magharibi na Amerika ya Kasikazini) zifanane kimaadili na jamii kutoka katika nchi ambazo zina mila na desturi za kimakabila au dini kama vile Afrika, Amerika ya Kusini na Asia. Ndiyo maana wakati wa kuandika mikataba hiyo ya kimataifa waasisi wa mataifa mbalimbali waliliona hili na kuweka maangalizo (reservatiojns) ya kuheshimu uwepo wa mabila, dini, mila na desturi zilizomo ndani ya mataifa ya Afrika, Asia na Amerka ya Kusini.

Tukianza na Ibara ya 27 ya Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Kiraia na Kisiasa (International Covenant on Civil and Political Rights, General Assembly Resolution 2200A, XXI of 1966), inasema nchi ambazo zina makabila, dini, mila, lugha za makabila zitakuwa na wajibu wa kulinda lugha, mila, maadili na dini za jamii zao!

Ibara ya 2 ya Mkataba wa Kimataifa kuhusu Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni(Convention on Economic, Social and Cultural Rights,) inasema katika kulinda mila, tamaduni, dini, lugha na maadili ya jamii, mataifa husika yakuwa na wajibu wa kutunga sheria zinazotakiwa kuvilinda visipotee!
Ibara ya 3 ya Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organisation, ILO) ikifafanuliwa katika waraka ujulikanao kama “Worst Forms of Child Labour No. 182 of 1999” inasema kwamba ajira mbaya kuliko zote kwa mtoto (worst form of child labour) ni pamoja na kumpa kazi au kumweka mtoto katika mazingira ya kazi yenye kumuathiri ukuaji wake kimwili, kiakili na kimaadili!

For the purposes of this Convention, the term the worst forms of child labour comprises “work which, by its nature or the circumstances in which it is carried out, is likely to harm the health, safety or morals of children”.
Maelekezo ya ILO kwa Serikali Wanachama No. 190 kuhusu namna ya kutafsiri Ibara ya 3 yaani “Worst Form of Child Labour” inazishinikiza serikali kuchukua hatua kali za kuzuia kazi hatarishi za mtoto kwamba lazima zikatazwe ambapo imezifafanua kazi hizo kuwa ni zile kazi ambazo kwa asili yake au mazingira yake ya kiutendaji zinaweza kuathiri afya, usalama, au maadili ya mtoto.

Pia, Ibara ya 32 ya Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Mtoto (United Nations Convention on the Rights of the Child (CRC) wa 1991 inayalazimisha mataifa yote duniani kutambua haki ya mtoto kulindwa dhidi ya unyonyaji wa kiuchumi na dhidi ya kufanyishwa kazi yoyote ambayo inaweza kuwa hatarishi au kuingilia elimu yake au kuwa yenye madhara kwa maendeleo ya afya yake kimwili, kiakili, kiroho, kimaadili na kijamii.

Ibara ya 2 ya Mkataba wa Kimataifa dhidi ya Vitendo Halaiki (UN Convention on the Prevention and Punishment of the Crime of Genocide, 1948(Genaral Asembl Resolution 260A (iii) of Dec. 1948) ambao ulianza kufanya kazi 1951 inasema pamoja na mambo menginbe kuiingizia jamii fulani tabia mpya ambazo zitaathiri na kupoteza mila na desturi za jamii tofauti ni kosa la halaiki (Genocide) na hivyo ni international crime.

Ibara ya 17 of African Charter on Human and People’s Rights inasema mataifa ya Afrika yatakuwa na wajibu kulinda mila, desturi, maadili na dini za mwafrika.

Uchambuzi
Hakuna haki mbili zinzazopingana zinaweza kukaa pamoja! Tumeona kwamba Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni ni haki za msingi za binadamu kama zilivyo Haki za Kiraia na Kisiasa. Kama hivyo ndivyo haki hizi, sheria na serikali za mataifa yote vina wajibu wa kuzilinda haki hizi ili zisihujumiwe.

Kwa maana hiyo, yatufaa kujua au kutambua kwamba dini zetu, vilugha vya makabila yetu, mila za makabila yetu, maadili ya makabila yetu, tamaduni za makabila yetu na mengine mengi ambayo kwa ujumla yanajulikana kama“intangible cultural heritage of humanity” yaani urithi usioshikika wa binadamu. Hizi ni Haki za Msingi za Binadamu ambazo tunatakiwa tuendelee kuwa nazo kama urithi wa vizazi vyetu, na ni mali za kiutamaduni (cultural resources) ambazo zinamtenganisha mwanadamu kitabia na wanyama wengine. Haki hizi ni haki za msingi amabazo zinalindwa na Sheria za Kimataifa. Kwa maana hiyo haki hizi nazinastahili kuheshimika, kulindwa na kupewa mazingira mazuri yasiyoweza kuzitishia kutoweka kwenye uso wa dunia vizazi hadi vizazi.

Kwa Mujibu wa Haki hizi tukija hapa Afrika, ni msimamo wa maadili, mila, imani, dini, desturi na utamaduni wa Mwafrika kwamba mwanaume haingiliwi na mwanamme mwingine kimwili! Huo ndio maimamo usiopingika wa Mwafrika!

Je, Afrika hakuna mashoga? Ninaposema Mashoga nikimaanisha watu wenye jinsia moja kujamiiana walikuwepo tangu enzi za Sodoma na Gomora, isipokuwa tabia hiyo ni tabia iliyokatatazwa(prohibited behavior) katika dini, katika utamaduni wa mwafrika na sheria za mataifa ya Afrika.

Kwa hiyo tabia hii ni tabia mbaya kimila, kidini na kisheria mbapo kimila na kidini tunaita uovu, na kisheria tunaita jinai (jinai).

Kwa sababu ni uovu, au jinai waliokuwa wanadhihirika kufanya mambo hayo wanakuwa wanastahili adhabu kama jinai nyingine kama vile wizi, uuaji, lugha za matusi, kupigana, kukwepa kodi, n.k.

Sasa mtandao wa ushoga au ndoa za jinsia moja vikihalalishwa, vitawekwa hadharani na hivyo jamii italazimika kuvikubali na kufuta dhana kwamba si uovu mbele za Mungu au mila zetu wala si jinai tena.

Sisi, au watoto wetu wenye kuamini katika mila, desturi au dini na ambao wanayo haki ya kupata mafundisho ya dini makanisani au misikitini yanayotuzuia mambo hayo ya ushoga kwa upande mmjoa lakini wakati huo huo Padre au Sheikh au Mzee wa Kimila au Mkuu wa Wilaya anafungisha ndoa mwanaume kwa mwanaume humo humo kanisani au msikitini, au kupokea mahari za kimila mwanamume anamchumbia manamume kwa upande mwingine, je, dini au mila au tamaduni zetu zitaendelea kuwepo?! Je, haki hizi zitakuwa zimelindwa na serikali kwa mujibu wa matakwa ya sheria za kimataifa? Katika mazingira gani?

Nchi za magharibi wameshafanikiwa kuhuisha sheria za kuhalalisha ushoga na ndoa za jinsia moja kwa kuongeza kipengele kwenye sheria dhidi ya ubaguzi kinachozuia kumbagua mtu kutokana na muelekeo wake wa ufanyaji mapenzi (sexual orientation). Kwa kosa hili, mashoga watukutu wamekuwa wakienda makanisani na misikitini kuomba kupewa sacramenti ya ndoa. Mapadre wanalazimika kufanya kuwahudumia wakiogopa kifungo kwa kosa la ubaguzi.

Where are our rights to religion, culture, moral values and other cultural heritage of humanity which we inherited from ancestors of our tribes?

Watetezi wa Ushoga wanadai kuwa mashoga waliharibika utotoni kutokana na mazingira magumu kijamii au kutokana na ulemavu kimaumbile na hivyo kulemaa kitabia na hivyo tuishi nao!

Hii mimi nakubalina nayo kuwa mashoga walio wengi hawakuzaliwa wakiwa mashoga bali waliharibika kutokana na mazingira mabaya wakiwa watoto,na wachache sana wana matatizo ya kimaumbile na kujikuta wanalazimika kuwa na tabia hiyo.

Hata hivyo katika maana ya jinai nakataa kwa sababu sheria za jinai haziulizi mazingira ambayo ulijikuta unapata tabia zilizokatazwa! Hata wezi kwa mfano haipingiki kwamba nao waliharibika kwa sababu ya mazingira magumu ya utotoni kama vile umaskini wa wazazi wao, au uyatima kutokana na vifo vya wazazi vilivyotokana na UKIMWI, viharusi, n.k ambavyo vilipelekea kukoswa malezi mazuri, njaa, na hatimaye kulemaa kitabia na kujikuta wanakuwa wezi, lakini wakiiba tunawafunga!

Au unakuta kuna tabia za wizi mtu anazipata kutokana na urithi wa kibaologia au vinasaba (phenotype genetical heredity) vya wazazi wake lakini tunawafunga bila kujali kuwa tabia zao za wizi ni ulemavu tunaendelea kuwatenga na jamii ili kuleta furaha kwa walio wengi.

Siku zote sheria, kwa mujibu wa Jeremy Bentham (1748-1832) na John Stewart Mill (1806-1873), zipo kwa ajili ya kuleta furaha kwa walio wengi na kuumiza walio wachache! Kwa mujibu wa nadharia hii hakuna sheria itakayokuja kutokea duniani yenye kufurahisha kila mtu haipo! Vivyo hivyo sheria zinazokataza ushoga zipo kwa ajili ya kulinda maadili ambayo pia ni haki za wasiokuwa mashoga ambao ndio walio wengi.

Nadharia hii ya Bentham na Mill haijapitwa na wakati hadi leo! Kwa kuthibisha msisitizo wa jumuiya ya kimataifa kuhusu haya, sheria za kimataifa zimeweka mipaka kuhusu uhuru wa mtu.

Katika falsafa ya sheria, kwa kuamini nadharia hii ya Bentham Mill, jumuiya ya kimataifa kupitia Ibara ya 19(3) ya ICCPR inatambua na inasema kwamba uhuru wa mtu utafurahiwa na mtu huyo kwa masharti na maangalizo maalum ambayo ni kwamba, katika kufurahia uhuru wake mtu hataruhusiwa kuingilia utu na heshima ya mtu mwingine, au kuathiri usalama wa nchi husika au kuathiri maadili ya jamii ya nchi husika! Hii sheria ina maana kubwa sana kuhusu kuweka mipaka ya uhuru wa mwanadamu kwa sababu wanasheria wanaamini kuwa “a human being was born unrealistic in nature and he needs law to engineer him socially”. Kwa maana hii hata kama mtu anao uhuru binafsi lazima uhuru huo uwe na mipaka kulingana na Ibara hiyo ya 19(3) ya ICCPR.

Uzuri zaidi nchi zote duniani zinatunga au kuweka katika katiba zao kutokana na maelekezo ya sheria za kimataifa hasa ICCPR! Hivyo si utetezi mtu kusema anao uhuru binafsi bila mipaka, haipo duniani kote!

Wabakaji wengi wana matatizo ya kibaiyolojia au kimaumbile kwenye “homornal imbalance with excessive libido and testosterone acting as the inhibitor of proper function of Central Nervous System at the time of rape” lakini tunawafunga tena vifungo vya maisha bila kujali kuwa nao matendo yao ya ubakaji ni kutokana na “automatism”!

Pili watetezi wa ushoga wanadai kuwa mtu ana uhuru binafsi ali mradi haathiri mwezake!Hii ni sawa kweli kama hauathiri mwenzako haina shida na ndiyo nadharia kuu ya sheria kwamba usimdhuru jirani yako na wajibu wa kujali (the principle of do not injure your neighbor and you shall not breach a duty of care)! Nadharia hii inasema binadamu anaweza kufanya kitendo chochote cha kumfurahisha alimradi asimbughudhi jirani yake na anao wajibu wa kujali majirani. Jirani katika sheria maana yake ni mtu yeyote yule ambaye anaweza kuathirika kutokana na matendo yako na ambaye unatakiwa kuchukua jitihada za kibusara kuelewa madhara ambayo yananaweza kumpata mbeleni kutokana na matendo yako (reasonable foresee-ability).

Watetezi wa ushoga wanasema ni “personal liberty”. Wanadai kwamba mtu anao uhuru wa kufanya mwili wake anavyotaka kwani hamwathiri jirani yake.

Swali ni je, ushoga unatuathiri sisi ambao siyo mashoga?

Athari za kisheria si lazima mtu atokwe damu, aumie kimwili, au apate hasara ya kifedha, bali hata athari za kisaikolojia, na kihisia (emotional injury)! Kwa mfano mtu angependa kutembea uchi barabarani, lakini je, jamii iko tayari kuona uchi wake hadharani, ukizingatia “emotional injury” kwa watu?

Je, watoto watakaozaliwa na kukuta watu wanatembea uchi bila nguo, watakuja kujua kuwa kuna wajibu wa kuvaa nguo? Jibu ni hapana.

Au mfano mwingine wa “personal liberty” swali ni je, mtu akiamua kujiua hadharani haina athari kwa watu wanaomshuhudia akijiua?

Au je, mtu anaweza kuwa nyumbani kwake yuko uchi, mara jirani akimgongea kutaka kuingia ndani, kwa nini mtu huyo avae nguo kwanza kabla ya kumfungulia mlango jirani huyo? Jibu ni kwamba, kitendo cha muonaji au jirani kuona uchi wa mtu huyo kinamfanya jirani kupatwa na hisia hasi na hivyo ni athali za kisaikolojia au kihisia (psychological or emotional injuries) ambazo jamii inabidi ilindwe dhidi ya matukio yenye uwezo wa kuiletea athari za namna hiyo vikiwemo vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja.

Vivyo hivyo, jamii zetua za kiafrika hazitaki na zinaathirika kuona mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja na hivyo wanaofanya hivyo wasituoneshe tabia zao.

Tofauti na sheria, katika maadili au dini inatosha kabisa kwa mtu ambaye hata kama akivunja maadili ya jamii au dini na akawa anafanya uovu wake kisirisiri, na kuiaminisha jamii kuwa tabia yake ni safi sambamba na jamii inavyotaka kumuona, basi jamii au dini zinaamini kuwa Mungu wake atakuwa anamwona na atamhukumu baada ya kifo chake.

Kwa maana hiyo, kwa sababu ushoga ulikuwepo tangu enzi za Sodoma na Gomora, basi mashoga hao waendelee kufanya mambo yao gizani ili wasituathiri sisi kihisia tusije tukatelekeza misingi ya mila, desturi, maadili na dini zetu vitu ambavyo tunayo haki ya kisheria kuendelea kuwa navyo!

Kwa sababu mwafrika akiona au kusikia au kuhisi mwanamme anaingiliwa na mwanamme mwenzake anaathirika kisaikolojia au kihjisia, hali hii ikizoeleka itapelekea kutoziamini na hatimaye kuzitelekeza mila, dini, desturi na maadili yake, mambo ambayo yanalindwa na sheria za Kimataifa na yanatakiwa kurithishwa kutoka vizazi hadi vizazi ili yasije yakapotea!

Ndiyo maana katika shule za Afrika kuna adhabu za viboko tofauti na Ulaya.
Hii ni kwa sababu elimu ya Mwafrika inaenda kwa njia mbili (dual traffic education) yaani kufundishwa academics ikiambatana na morality wakati elimu ya Mzungu inaenda kwa njia moja, (single traffic education) yaani ni academics and “let it go alone”(yaani liache liende peke yake) au mimi naweza nikasema ni “untamed mankind.”

Barani Ulaya, ukiachana na malezi yao ya elimu bila viboko au kwa lugha nyingine Uhuru wa Watoto uliopelekea kupotea kwa maadili, pamoja na mambo mengine ushoga unashamiri kwa sababu ya kukithiri kwa mfumojike (feminism).

Mtoto wa mtu (binadamu) kwa asili yake anazaliwa akiwa na akili ambayo haijui chochote kinachoendele duniani (tabulla rasa). Hivyo anapoendelea kukua anaweza kujifunza tabia ambazo jamii inaweza kuziona ni machukizo na hivyo huhitaji ukaribu wa mzazi au wazazi wake na kadri anavyozidi kuelekea kwenye kufikia umri wa kujitambua au mabadiliko ya kibiolojia ndivyo anavyozidi kuhitaji sana ukaribu zaidi wa wazazi wake kumpanga asije akaharibika kitabia. Hivyo mafundisho ya wazazi ikibidi yenye kuambatana na adhabu ya viboko ni muhimu sana katika kuwaanda kuwa na tabia zinazokubalika katika jamii.

Kwa kifupi, tofauti na mnyama, kimaumbile, mtoto wa binadamu tabia zake zinatokana na mambo mawili ambayo ni mazingira (environment or experience) anayoishi na asili yake ya vichoicheo vya fahamu (intuitions); wakati mnyama tabia zake anakuwa nazo kutokana na intuitions pekee. Ndiyo maana mbuzi wa New York, mbuzi, wa India, mbuzi wa Tarime, mbuzi wa Ludewa na Mbuzi wa Dar es Dar es Salaam wote wana tabia sawa, wakati binadamu wanaoishi katika maeneo tajwa lazima wawe na tabia tofauti.

Kwa maana hiyo tukubaliane kwamba malezi ya watoto yatokanayo na wazazi, wakiyakosa wakiwa wadogo (lack of parental guidance) watajikuta wameshapotea kitabia zikiwemo tabia za uelekeo wa kujamiina! Hii ndiyo maana zamani kidogo watoto walipomaliza kunyonya (post-lactaion) waliwekwa karibu na mabibi/mababu zao kwa ajili ya kujitambua kijinsia (social differentiation).

Tatu, kushamiri kwa mfumo jike (feminism) katika bara la Ulaya na Amerika ya Kaskazini ambao unakua kwa kasi duniani kote ikiwemo Afrika kumepelekea watoto wa kiume katika kukua kwao kumwogopa mtoto wa kike kimahusiano ya kijinsia na hivyo mtoto wa kiume kukua akiwa na hofu dhidi ya mahusiano ya kimapenzi kutokana na adhabu kali za kisheria na vifungo vya jela kwa wanaume wanaoingilia wanawake. Hii ni kwa sababu sheria zimeweka mazingira mapana mno ambayo hata hayana sura ya kutumia nguvu lakini zikayatafsiri kama ubakaji. Kwa hiyo mwanamke amekuwa ni wa kuogopwa kijinsia hivyo watoto wetu wa kiume wanajikuta kujaribiana wao kwa wao wanapofikia umri wa mabadiliko ya kibaiyolojia.

Matokeo yake, hata hapa Tanzania, tumeanza kujionea jinsi idadi kubwa ya watoto wa miaka chini ya 12 wa kike na wa kiume wakilawitiwa au kubakwa na watu wazima (child molestation) ambao, kwa sababu ya kushindwa kumshawishi mwanamke mwenye umri unaofaa au kumwogopa kutokana na wanawake kupenda pesa ambayo anakuwa hana, au kwa hofu ya kufungwa hivyo kumbaka mtoto akiamini mtoto hataweza kusema.

Aidha watoto wa kiume pia wanakuwa hawana ushawishi wa kimapenzi kwa wanawake wanaowazidi umri yaani wenye umri wa miaka 18 au zaidi kama sheria inavyotaka. Kwa mfano, mvulana wa kiume mwenye umri wa miaka 15 hawezi kumshawishi msichana mwenye umri wa miaka 19, n.k.

Kutokana na kutojamiiana kwa muda mrefu, watoto hao wa kiume wanajikuta wanapatwa na “temporary insanity” inayotokana na “automatism” inayotokana na hormones za mapenzi kusongamana kwenye damu.

Haya mambo ni ya kibaiolojia na yanaweza kusababishwa na “high levels of sexual hormones in their plasma” na kuamua kuingiliana bila kujali kuwa ni jinsia moja. Kwa mujibu wa taarifa zilizoko kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), angalau watoto mia sita (600) chini ya miaka 12 wanabakwa na kulawitiwa tena na wanaume walioko karibu na familia za watoto hao.

Kwa mujibu wa Patrick Devlin (1905-1992) katika kitabu chake kinachoitwa “The Enforcement of Morals” (1959) anasema kwamba “the general convictions and judgements of the society about a certain phenomenon is where legal decisions must be rested”; yaani mtazamo na mapenzi ya kimtazamo ya jamii kwa ujumla kuhusu jambo fulani ndipo maamuzi ya kisheria yanapotakiwa kuungana.

Sasa jamii yetu haipendi uchafu huo na sheria hazitambui uchafu huo hivyo wanaharakati, au serkali, au kikundi cha watu au mtu yeyote hana mamlaka ya kushinikiza mataifa yetu kupokea uchafu huu! Wanatuonea.

Hitimisho
Wimbi la ushoga na ndoa za jinsia moja linazidi kupanda kwa kasi duniani na watu bila kujua au kwa kupuuza madhara ambayo mtandao huu unaweza kuyaleta kwenye jamii zetu wanazidi kushabikia kwa mkumbo, hii ni hatari sana! Mimi nasema hii ni vita takatifu (bellum sanctus) hivyo hiki ni kizazi ambacho kila mtu anatakiwa aishike sana imani yake.

Tunao wajibu wa kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya watoto wetu kwa maana sisi ndio wazazi wa kizazi hiki. Na hivyo kama wazazi wetu walipambana kuturithisha maadili, mila, desturi na dini walizorithi kutoka kwa mababu zetu na sisi pia tunao wajibu wa kuwaandalia na kuwatunzia watoto wetu mazingira mazuri ya kuwalea, kuwafunda na kuwarithisha imani zetu! Tutajiteteaje kwa Mungu kwa kuwaachia watoto wetu dunia chafu?

Baba mwema huwapigania watoto wake ili kuwaweka katika sehemu salama kiafya, kimwili, kiakili, kiroho na kimaadili (a good father leaves a better place for his children)!

Na serikali zote duniani zinawajibika kwa kiwango cha hali ya juu kisheria kutuwekea mazingira mazuri ya kulinda na kurithisha imani zetu ikiwemo kuzuia kwa gharama zote ushoga na ndoa za jinsia moja vizazi hadi vizazi.

Sasa tunakwama wapi waafrika kushindwa kujitetea dhidi ya fedheha tunayotwishwa na weupe wakati sheria za haki za binadamu na za kimataifa viko upande wetu? Au mzungu amefikia kiwango hicho cha kuidharau Afrika kwa sababu ametuelewa kwamba hatuna hata akili ya kujengea hoja sheria zinazotupatia haki zetu? Serikali zetu zitutetee dhidi ya ujinga huu kwa kweli.

Mwenyezi Mungu awabariki na kuwalinda!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
100 %
Surprise
Surprise
0 %