0 0
Read Time:2 Minute, 21 Second

The Tanzania Think Tank.

Moja ya mijadala mikubwa ambayo imetawala duniani kote kwa wiki nzima ni suala la Urusi chini ya Jasusi Vladmir Putin kutangaza kuishusha dola ya Marekani sokoni na kuanza kutumia Yuan ya China katika biashara zake!Tamko la kwanza la wazi la Moscow baada ya vikao na ziara ya Rais wa China XI Jinping Nchini Urusi mapema Mwaka huu!

Ajenda ya Marekani kuhusu “Ushoga” kwa maana mapenzi ya jinsia moja pia umeenda kutishia mahusiano yake ya kiuchumi na kisiasa dhidi ya Nchi nyingi za Africa!Juzi Marekani imeitishia Nchi ya Uganda iachane na kupitisha Sheria ya kupambana na “Ushoga” na kutishia kuitangazia kuiwekea vikwazo.

Rais Vladmir Putin jana akiwa NCHINI Afrika Kusini alitumia muda wake mwingi kupinga sera ya Marekani kuhusu Mapenzi ya jinsia moja ndani ya bara la Afrika!Ni wazi kuwa Urusi inatumia policy ya devide them and rule them kwa Marekani dhidi ya Afrika!

Zaidi ya asilimia 50 ya biashara ya Afrika kwa sasa inafanya na Nchi ya China na kuna uwezekano mkubwa Nchi ya China kuendelea kuwa mhimili Mkuu wa biashara na mahusiano na Afrika hasa kupitia mikopo katika miradi mingi ndani ya bara la Afrika!

Rais Vladmir Putin wa Urusi juzi akatangaza kufuta madeni yake yote kwa Nchi za Afrika!Unajua hii ina maana gani?Moscow inajaribu kutaka kuidhoofisha Nchi ya Marekani ndani ya bara la Afrika huku Marekani ikijaribu kufanya hivyo hivyo kumdhoofisha Rais Vladmir Putin kupitia Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu yaani ICC.

Katika mpasuko huu mkubwa wa kisiasa, Mataifa mengi ya Afrika ambayo biashara zao nyingi zinatumia dola ya Marekani,yanaweza kuathirika leo kesho au baadae!kwa ujumla Uchumi wa “Currencies” unaweza kuporomoka sana duniani kufuatiwa kuwepo kwa hatari au tishio la”medium of transaction shift”.

NINI TUNASHAURI KWA NCHI YETU TANZANIA?

I.Uchumi dhahabu pekee yake ndio ambao unaweza kutufanya kuwa stable leo kesho na baadae!Mabadiliko yoyote ya medium of exchange duniani yawe ya “Dola o,Yuan or Paundi” hayawezi kuaffect “Foreign Reserve” yetu kama tutakuwa na National Gold Reserve ya kutosha!

II.Kwa maslahi mapana ya Usalama wa Kiuchumi,Tanzania inapaswa haraka kuwa na Banki za Madini katika kanda zetu zote za B.OT kuanzia Kusini,Kaskazini,Kanda ya Kati,Nyanda za Juu Kusini na kadhalika!Hiyo sio option kwa sasa bali suala la kufa na kupona!Tumeona hatari ya kuwekeza katika Uchumi wa fedha pekee “Currencies”.

III.Hatari ya kuwekeza kwenye Uchumi wa fedha hasa kwenye Foreign Currency Reserve “inalimit” uwezo wetu wa kununua bidhaa nje ya Nchi!Kwa mujibu wa Repoti ya BOT ya Mwezi Desemba,2022 inasema,Tanzania ilikuwa na uwezo wa kununua bidhaa nje ya Nchi kwa miezi minne pekee!(4.5 months).

Ushauri wetu huu tunaomba ufanyiwe kazi na Serikali haraka kwa maslahi mapana na Usalama wa Taifa letu,Tanzania!

George Michael Uledi.
Mwenyekiti wa Jukwaa.
The Tanzania Think Tank.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %