0 0
Read Time:52 Second

Italian government seeks to penalize the use of English words

Rome, Italy

Serikali ya Waziri Mkuu Bi. Giorgia Meloni wa Italia ina mpango wa kuwalipisha faini Waitaliano wote watakaotumia maneno ya Kiingereza au lugha nyingine yoyote ya kigeni katika mawasiliano au nyaraka rasmi.

Sheria hiyo itawataka watu wote wanaofanya kazi kwenye utawala wa umma kuwa na uwezo wa kusoma, kuandika na kukimudu Kiitaliano.

Wale watakaoenda kinyume na sheria hiyo watalipa faini ambayo inaweza kufikia kiasi cha euro 100,000.

Pamoja na kuwa mpango huo unajumuisha lugha zote za kigeni, hata hivyo unailenga zaidi lugha ya Kiingereza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama cha Brothers of Italy ambao ndio waanzilishi wa muswada huo, matumizi ya maneno ya Kiingereza yanakidhalilisha na kukishushia hadhi kiitaliano.

Mswada huo utapelekwa Bungeni kwa majadiliano.

https://www.cnn.com/2023/04/01/europe/italian-government-penalize-english-words-intl

https://beta.ctvnews.ca/national/world/2023/4/1/1_6338822.amp.html

https://www.reuters.com/world/europe/melonis-party-looks-shield-italian-language-foreign-contamination-2023-03-31/

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %