0 0
Read Time:2 Minute, 7 Second

Na Zain

Diaspora USA

IJUE HADHI MAALUMU

Kimfaacho mtu chake!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan

Hadhi Maalumu ni kutambuliwa rasmi kwa wanadiaspora wa Tanzania wenye uraia wa nchi za nje na serikali ya Tanzania. Utambuzi huu unawahusu pia familia na vizazi vyao.

Watatambuliwa kwa vitambulisho vya kielektroniki vitakavyotolewa na serikali ya Tanzania.

Uzito wa vitambulisho hivyo utayafanya mataifa mengine ulimwenguni kuvithamini vitambulisho hivyo. Vitatambulishwa duniani viheshimike.

Vitambulisho hivyo vitaambatana na kushughulikia matatizo ya haki za kiraia hasa katika maombi maalumu yaliyowakilishwa na wanadiaspora kwa serikali vikiwemo umiliki wa ardhi na kuwekeza Tanzania sawa na raia wengine wa Tanzania.

Hadhi Maalumu sio adhabu kwa wanadiaspora wa Tanzania, ni jawabu zuri la kitendawili cha madhara ya uraia pacha. Hadhi maalumu ina faida za uraia pacha na inaepuka madhara yake.

Hadhi Maalumu ina faida nyingi zikiwemo hizi;

  1. Inaifungua Tanzania kwa wanadiaspora wake wenye uraia wa nchi za nje bila ya kutoa uraia pacha kwa raia wa mataifa ya nje.
  2. Inazuia raia wa Tanzania wenye asili ya nchi za kigeni kuchukua uraia pacha kihalali na nchi za nje au kwao. Wakiruhusiwa wanaweza kuhamisha mali nje ya nchi kihalali. Hili ni kundi la matajiri na wamiliki wa uchumi wa Tanzania kwa kiasi kikubwa sana.
  3. Inailinda serikali isopoteze kodi na faida za wawekezaji wa kigeni. Ieleweke kuna wewekezaji tayari wako Tanzania zaidi ya miaka kumi, na hata wawekezaji wapya wakikaa nchini muda mrefu watakuwa na haki ya kudai uraia pacha kama utakuwa umeruhusiwa Tanzania.
  4. Inawalinda wananchi wa Tanzania kushea fursa za kiuchumi na raia wa kigeni. Kwenye hili ardhi ya migodi, mashamba, biashara, nafasi za kazi, elimu, bahari, uvuvi nk, vinahusika. Raia wa kigeni katika kundi hili ni pamoja na wakimbizi na raia kutoka nchi jirani hasa maeneo ya mipakani.
  5. Inalilinda taifa zima kuathiriwa na wageni kimaadili, utamaduni, uhalifu, na mengineyo, hata lugha ya kiswahili haitatosha au itafunikwa.

Kwenye Clubhouse hata loya “msomi” akikuambia Tanzania inaweza kutoa uraia pacha kwa wazawa tu anakudanganya. Ndoa hata za kufeki, kuzaliwa Tanzania, ukazi wa muda mrefu na vigezo vingine vinatoa uraia kwa raia wa kigeni. Kinachowakwamisha hivi sasa kuchukua uraia wa Tanzania kwa wingi ni sharti la kuukana uraia wa kwao ili wapate uraia wa Tanzania.

Kumbuka pia wanadiaspora wa Tanzania wanaochukua uraia wa nje wengi wao ni maskini wako nje kuganga njaa, raia wa kigeni watakaochukua uraia Tanzania ni matajiri. Hata wakiwa wachache, haihitaji matajiri wengi kumiliki kila kitu na kuwakosesha fursa za kiuchumi watanzania wengi pamoja na wanadiaspora wao.

Tahadhari kabla ya hatari, usijeambulia cheti cha ndoa, mke kachukuliwa!

Kazi iendelee!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %