0 0
Read Time:52 Second

WU® MEDIA

Hiba Abouk star wa sinema adai nusu ya Mali ya Hakimi

Hiba Abouk, Mcheza Filamu Maarufu Nchini Hispania ambaye ni Mke wa Mchezaji wa PSG ya Ufaransa Achraf Hakimi,akiwa Mahakamani kushughulikia Kuachana na Hakimi (Divorce), Hiba ameomba apewe Nusu ya Mali za Hakimi

Lakini Mahakama imemtaarifu Kwamba Hakimi Ni Mtu kapuku tu kwani Hana Mali yoyote ile, Hana Magari, Hana Nyumba, Hana Mashamba Wala Hana Vito vya thamani Kama Cheni za dhahabu, Saa n.k, kwani Vitu na Mali zote Makabrasha yanaonyesha Zimesajiliwa kwa jina la Mama yake Mzazi. (Mama Hakimi), Hakimi Hana hata Nguo zenye Jina lake.

Mahakama imeendelea kumtaarifu Hiba Kuwa Hata Mshahara wa Hakimi ambao Ni Euro Milioni Moja kwa Mwezi, zaidi ya Bilioni 2.5 za Kitanzania Asilimia 80 ya Mshahara huo huwa unawekwa kwenye account ya Benji ya Mrs Fatima Yaani !(Mama Hakimi).

Kwa Sasa Hiba Abouk Anaendelea kushauriana na Wanasheria Wake kuhusu Hatua gani za kisheria za Kumchukulia Kapuku Hakimi.

HAKIMI AKIMBUSU MAMA YAKE BAADA YA KUFUNGA GOLI KWENYE KOMBE LA DUNIA LA QATAR
READ
Happy
Happy
100 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %