0 0
Read Time:1 Minute, 7 Second

WU® MEDIA

Dodoma.

Tanzania ina jumla ya Diaspora 1.5 milioni, Bunge limeelezwa leo. Idadi hiyo imetajwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati akijibu swali la Mbunge wa Mikumi, Dennis Londo leo Ijumaa Aprili 14, 2023.


Londo ametaka kujua Tanzania ina diaspora wangapi na ni upi mchango wao katika uchumi wa nchi na kama kuna mpango wa kuwapatia hadhi maalumu.
Naibu Waziri amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba 2022, Diaspora wa Tanzania walituma nchini kiasi cha Dola za Marekani 1.1 bilioni ambayo ni sawa na Sh2.6 trilioni.
“Vilevile, katika kipindi hicho diaspora walifanya uwekezaji kupitia ununuzi wa nyumba na viwanja wenye thamani ya Sh4.4 bilioni na ununuzi wa Hisa zenye thamani ya Sh2.5 bilioni,” amesema Mbarouk.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri, kwa sasa Wizara inakamilisha mfumo wa kidigitali wa uandikishaji wa Diaspora (Diaspora Digital Hub), unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni 2023 mfumo huo aliosema ni endelevu utawezesha ukusanyaji endelevu wa takwimu za Diaspora.

Amesema diaspora huchangia katika maendeleo ya nchi kwa kutuma fedha za kigeni nchini (Remittances), kuwekeza, kuleta mitaji, utaalamu na Teknolojia inayoweza kuchangia kukuza uzalishaji wa mazao, bidhaa na huduma mbalimbali zenye tija kiuchumi.

Serikali pia imesema diaspora hutangaza fursa za kiuchumi, biashara, utalii na uwekezaji zinazopatikana nchini.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %