0 0
Read Time:4 Minute, 14 Second

BARABARA YA KUELEKEA UPORAJI WA RASILMALI ZA BARA LA AFRIKA.

George Michael Uledi.
Kyela, MBEYA.
April 24,2023.

Kufikia mwaka 2040 bara la Afrika litakuwa koloni tena na WB,IMF na China,safari hii Scramble & Partition ya bara la Afrika itakuwa kupitia kitu kinaitwa mtego wa madeni “debt trap diplomacy”.Kizazi cha Vijana Wasomi wa Afrika ndani ya Academia,ndani ya Siasa na ndani ya wanaharakati lazima tupaze sauti sasa!

Read Diplomacy

Wakati mafahari wawili duniani yaani Marekani na China wakipambana sasa kufikia matamanio makubwa ya uchumi kwa Mataifa yao kwa mgongo wa Afrika then Afrika inapaswa kijihoji,kujikagua na kuamua kama inapaswa kuendelea kutumiwa na kuingizwa kwenye debt trap na Mataifa ya kibeberu na vyombo vyao vya fedha yaani WB & IMF.

Dunia inajua wazi kuwa ndani ya miaka kumi kuanzia sasa(2033),China ndio itakuwa Nchi yenye Uchumi mkubwa duniani baada ya “kuiovertake” Nchi ya Marekani na katika kutimiza lengo hilo la kufa na kupona kwa China, bara la Afrika inakadiliwa kuwa mgongo wa kufikia lengo hilo angalau kwa asilimia 60%.

Taif la Marekani pia limekuwa likitumia vyombo vyake vya Kimataifa vya FEDHA kama WB & IMF kutekeleza dhana nzima ya “debt trap diplomacy” kwa targeted economies!Vita ya giants wawili inachezwa barani Afrika na bahati mbaya wanasiasa vipofu wa Afrika wanademka vizuri kabisa!Kenya kama “Samba” imeshaanza kukolea!Ruto na Serikali yake wanalia!

Tanzania yangu inapaswa kwenda na akili kubwa kwenye kusoma mchezo huu mchafu wa Mataifa makubwa dhidi ya raslimali zetu muhimu kwa maslahi ya vizazi vya baadae!Mikopo ya WB & IMF kwa Tanzania ni kitanzi kikubwa kwa Usalama wa baadae wa Taifa hili!

Wenye “macho makubwa na akili kubwa” wanajua kuwa mradi wa Bandari ya Bagamoyo wa China-Oman kwa mfano utakuwa ni sawa na kujipiga pingu mbili za Mabeberu wawili yaani Marekani na China kwa wakati mmoja!Mabeberu wote hawa wanataka kuitumia Afrika kufikia malengo yao ya muda mrefu kama Mataifa makubwa duniani!


Increasing debt in many African countries is a cause for worry
READ

TANZANIA NI MOJA KATI YA “TAGETI” MUHIMU BARANI AFRIKA KUFIKIA MALENGO YA WAKUBWA HAWA!

I.GDP ya Tanzania inaweza kuwa ndio GDP ya tatu kwa ukubwa barani Afrika kufikia Mwaka 2040 baada ya ile ya Nigeria na ile ya Afrika Kusini!Uwepo wa rasilimali nyingi muhimu ndani ya Taifa hili kunavifanya Vyombo vya Kifedha duniani kama WB & IMF kuiweka Tanzania kama “target” katika mpango wao.

Uwepo wa Miradi ya LNG,Rare Minerals,giografia nzuri ya Tanzania,GDP inayokuwa kwa kasi ndani ya Afrika, ardhi kubwa na mambo mengine mengi kunaifanya Nchi ya Tanzania kupewa kipaumbele zaidi na vyombo vya fedha duniani kwa malengo maalum!Rejea mradi wa One Belt One Road Initiative wa China kuhusu ujenzi wa Bandari Duniani!Bandari ya Bagamoyo ni TAGETI muhimu mno katika kuifanya China kuwa Super Power in ten years to come!

II.Njia pekee ya kuiweka mateka Tanzania ni kwa kupitia debt trap diplomacy!Mwezi jana Waziri wa Fedha PhD Mwigulu Nchemba alitangaza uwepo wa taasisi ya Kimataifa ya kupima ustahimilivu wa madeni ya Taifa duniani na jamaa wale wakaja na report kuwa Nchi ya Tanzania inakopesheka big time!Nataka niweke clear hapa kuwa sipingi Nchi kukopa lakini nataka kuonya kuwa mchezo huu wa Mabeberu sio salama sana kwetu kwa baadae”hidden agenda”.

Ni bora sana kusitisha baadhi ya miradi mikubwa ya Kimkakati kwa sasa kwa lengo la kupunguza kukopa!Mchumi mmoja Nguli duniani,katika Mahojiano yake na Gazeti la The Citizen la Mwezi Februari,2023 aliionya Tanzania kuhusu kutekeleza miradi mikubwa kwa wakati mmoja tena kwa kutumia fedha za IMF & WB!Ni hatari sana!

Na Mimi leo nataka niionye Serikali yangu ya CCM kwamba Usalama wetu kama Chama dola utategemea sana ni kwa jinsi gani tunaweza “kuanalyse”na kuweza “kuanticipate” matukio yajayo kwa Usalama wa Chama chetu!Kama kwa Mfano kama Uchaguzi Mkuu utafanyika Kenya leo ni wazi kwamba Serikali ya Kaka yangu William Rutto inakwenda kushindwa Uchaguzi asubuhi na mapema!
Ishu kubwa itakuwa ni deni la Taifa,madeni madeni madeni!

III.Kuna siku tutakabana mashati hapa na Serikali ya Awamu ya Saba Miaka ya 2030 kwenda mbele na labda PhD Mwigulu Nchemba atakuwa hayupo kwenye Serikali hiyo!
Chama cha mapinduzi kama ambavyo Kaka yangu na KM wangu wa CCM Taifa anasema,”sisi ndio wenye duka…wakina Mwigulu Nchemba ni wauzaji wa duka la CCM”.

Pale Kenya tayari duka limefilisika baada ya kutekeleza miradi miwili tu ya SGR na Mradi wa Bandari ya Lamu na Mombasa kwa mikopo ya China!Serikali ya William Rutto haiwezi kutoboa kwenye Uchaguzi ujao kwa maana madeni ya Kenya hayawezi kuisha leo wala kesho!Kuna miaka kumi mpaka kumi na tano ya kuservice madeni yale!

Mwenye duka CCM anapaswa haraka kuanza kumuuliza muuza duka wake Serikali kama kweli duka letu linaweza kuendelea kuwepo kwa miaka ishirini mbele kwa kuchukua reference ya Kenya!

Wajibu wangu kama kada-kijana wa CCM ni kuweza “kuanticipate” matukio ya kidunia ambayo yanaweza kuwa na matokeo hasi katika kutunza dola yetu kwa miaka ya baadae na hiyo hasa ndio kazi ya Political Strategist yoyote duniani!

To anticipate,to justify anticipations and finally is to shout.

+255746724684.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %