0 0
Read Time:2 Minute, 31 Second

WU® MEDIA

Na Zain

Nicheke nina mbavu?

Ile kesi watu wamepigwa na hata ukitokea muujiza wakashinda mahakamani hawawezi kupata uraia pacha Tanzania, kwa sababu mahakama haitungi sheria mpya.

Kesi yenyewe pia imekaa kimagumashi, sasa hivi ina hatari ya kufutwa kwa sababu ya pingamizi tatu mbili zikiwa ni za kiufundi, kwa maana ya kuwa imefailiwa vibaya.

Hoja zao ni za vichekesho hata mimi nazijibu;

  1. Kuna wanaosema mtanzania hapewi Hadhi au cheo kwa nasaba, urithi au jadi. Kwa akili yao Hadhi iliyotajwa hapo ni Hadhi Maalumu na nasaba ni uzawa wa Tanzania. Wakijifunze kiswahili. Kimsingi hapo kinachosemwa ni mtanzania hapendelewi kwa kuwa ni wa ukoo fulani (nasabu) au ni mrithi wa nani. Isitoshe kifungu kinawahusu watanzania, Hadhi Maalumu haitolewi kwa watanzania.😂
  2. Wanaipinga sheria ya uraia ya Tanzania ya mwaka 1995. Wanasema haikuwa na haki ya kumuondolea uraia mtanzania, lakini hawasemi kuwa ni sheria hiyo hiyo ndio iliyoelejeza raia wa Tanzania ni nani. Ikifutwa maana yake hakuna raia wa Tanzania. Tutarudi kwenye uraia wa mkoloni.
  3. Duniani kote hata raia wa kuzaliwa, kutokana na sheria za nchi anaweza kupoteza uraia wake katika mazingira fulani na wakati mwingine ni automatically.
  4. *Automatic loss of citizenship * sio kinyume cha sheria wala demokrasia. Nchi zote duniani zinazopinga uraia pacha watu wakichukua uraia wa nje wanapoteza uraia wao wa kuzaliwa *automatically. * Kwa Holland hata ukikaa nje ya Holland miaka mingi bila ya kurudi Holland au hata ku-renew paspoti yako unapoteza uraia wao. Marekani ina vipengele saba ukifanya kimoja wapo unapoteza uraia hata wa kuzaliwa Marekani, ingawaje mahakama imeingilia hilo jambo, sasa imekuwa ni vurugu tu, case by case. Mahakama inapingana na Congress. Tanzania mahakama inaweza kupingana bunge?
  5. Wanasema wanawake hawana haki sawa kwenye sheria ya uraia ya Tanzania. Hili jambo hata likifanyiwa marekebisho linawapaje wao uraia pacha?
  6. Wanasema hawakupewa nafasi ya kujitetea kabla ya kunyang’anywa uraia wa Tanzania. Hawakupewa due process, sasa wakipewa hiyo due process, waruhusiwe kujitetea ndio watapata uraia pacha? Kwanza watajitetea nini, tulikuwa na njaa tukaona tuchukue uraia wa nje ili tupate chakula?
  7. Wanasema katiba ya Tanzania inatambua uraia pacha kwa sababu ina kifungu kinacholiruhusu bunge litunge sheria ya kumzuia mwenye uraia pacha asipige kura Tanzania. Hiyo sheria iliyotungwa iko wapi? Haikutungwa kwa sababu sheria ya uraia ya mwaka 1995 ilimfuta uraia mtanzania anaechukua uraia wa nje.
  8. Wanasema uraia wa kuzaliwa Tanzania haunyang’anyiki kwa sababu umetolewa na Mungu, ni wapi ambapo katiba au sheria ya Tanzania imesema uraia wa Tanzania haunyang’anyiki?
  9. Tuchukulie wameshinda wao madai yao yote, mahakama imeamua sheria irekebishwe au itungwe upya. Sheria imerudi bungeni, msimamo wa serikali ya Tanzania ni kutotoa uraia pacha. Mahakama haiwezi kuiambia serikali ya Tanzania ibadili msimamo wake, sana sana sheria ya uraia itarekebishwa, na bunge linaweza kutunga sheria nyingine kali zaidi ya kukataa uraia pacha.

Wamefungua kesi wakitegemea hawashindi, tegemeo lao ni mahakama ya Afrika ya mashariki, kweli mahakama ya Afrika ya mashariki inaweza kurekebisha sheria ya uraia wa Tanzania?

Na nani ana muda wa kusubiri mlolongo wote huo zaidi ya kiongozi wa kesi ya uraia pacha ambaye yeye ana uraia wa Tanzania? Wengine anawaburuza tu kufanikisha malengo yake binafsi.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %