
Na Mwana Habari wetu K.L
WU® MEDIA, Greece
Jumamosi 6/5/2023 watanzania wa Ugiriki walikamilishiwa zoezi la kukabidhiwa pasi . Zoezi hiili lilisimamiwa na Afisa wa diaspora wa ubalozi uliopo Rome. .Mhe Sigfred Nnembuka.

Jumuiya ya watanzania Ugiriki inapenda kutoa shukran zake za dhati kwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy ambae anawakilisha pia Greece na nchi zingine za ukanda huu Mh.Mahmoud Thabit Kombo.
Mh Balozi kama mlezi amekuwa karibu na Diaspora wa Tanzania kutafuta majawabu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Changamoto ya passport ilikuwa ni tatizo na kikwazo kikubwa kwa Watanzania nchini Greece, tunashukuru kwa kukamilika zoezi hili.
“Watanzania Wote tumefurahishwa Sana na tunamuombea Mh Balozi, Mola amzidishie baraka na moyo wa kuendelea kutusaidia.”
Mwisho tunawashukuru maofisa wote wa Ubalozi hasa kitengo Cha passport kwa shirikiano mliotupa katika kipindi chote Cha mchakato wa Maombi ya passport.

