0 0
Read Time:1 Minute, 39 Second

Na H.Mkali

“MBEGU ZA ASILI ZIHIFADHIWE NA KUZALISHWA KWA WINGI”

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imepokea ugeni wa Kampuni zisizo za Seriki zinazojishughulisha na uhamasishaji, uzalishaji na Utumiaji wa Mbegu za asili lengo ikiwa ni kujadili namna ya Kushirikiana katika kutafiti na kuhamasisha matumizi ya Mbegu za asili.

Kituo cha Utafiti cha Makutopora kimepoteza kabisa hadhi na haki ya kusimamia mbegu zetu za Asili.

Kwani hiki Kituo si ndo hicho cha Makutopora ambacho tangu 2016 kimejikita kwenye Utafiti wa Kilimo cha Uhandisi Jeni au GMO – ‘Genetically Modified Organism?’

Kweli ni busara kukabidhi mbegu zetu za asili Kituo hiki?

Kwani hizo mbegu zetu za asili zinatakiwa zifanyiwe utafiti gani ambao ni lazima ufanyiwe huko Makutopora?

Tafiti zenye kujitegemea (duniani kote) zimeonyesha waziwazi kuwa kilimo cha asili na cha GMO haviwezi kudumu mbega kwa mbega kwa sababu “contamination” kupitia upepo, wadudu na wanyama itauua kabisa hizo mbegu za asili.

Sasa leo, Taifa letu likabidhi mbegu zetu watu “wanaojiita wasomi/wanasayansi” na ambao wanasadiki kuwa (a) kilimo cha GMO ni kilimo bora (b) Na ni wanasayansi ambao wanaitongoza Serikali yetu ikumbatie hiki kilimo haramu cha GMO.

Hivi ni ngoma gani inachezwa hapa?

Watanzania fungueni macho.

TARI hivi sasa ipo kwenye makwapa, yaani inafadhiliwa na Taasisi na Mataifa ya nje ambayo hayasadiki kwenye mbegu za asili; Sasa Tanzania kukabidhi mbegu zetu Kituo hicho ni kuua mbegu zetu za asili.

Mfumo Rasmi?

Huu ni ulaghai na utapeli wa wazi wazi. Mbegu zetu za asili zipo kwenye mfumo rasmi tangu kilimo kianze hapa duniani, miaka takribani 10,000 iliyopita. Ni mfumo unaowaruhusu wakulima kuhifadhi, kupeana na kuuziana mbegu za kupanda msimu ujao. Na mfumo huu rasmi ndio ambao kilimo cha GMO kupitia hicho Kituo cha TARI cha Makutopora kinapiga vita.

Watetezi wa mbegu za Asili fungueni macho, mnaingizwa kichwa mtungini hapa.

Mfumo rasmi wa ku- “parent” mbegu ni wa kisaliti kwa sababu unafuta uhuru wa wakulima na kwa mwendelezo uhuru wa Mataifa wa Chakula.

mkali@live.co.uk.
07/05/2023.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %