WU® MEDIA, Greece
Watanzania Greece
Jumuiya ya Watanzania waliungana na familia ya Ndugu Kassa Mussa kwenye sherehe ya Maombi na Dua ya siku arobaini ya kuzaliwa mtoto wa Sharmila ambae ni Binti wa mwanasoka maarufu mstaafu wa Wagosi wa kaya Costal Union ya Jijini Tanga.
Sherehe hizo za arobaini zilizofanyika mjini Athens nchini Ugiriki siku ya Jumamosi tarehe 10/06/2023 zilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania nchini humo Mh. Kayu Ligopora.
Shughuli ilifanyika kwenye ofisi ya Jumuiya ya Watanzania na ilianza kwa kisomo na dua na kufuatiwa na pilau ya kukatana shoka pamoja na mikaango mingine iliyoandaliwa vizuri na kina mama
Umoja wa Watanzania umekuwa ni chombo IMARA kinacho waunganisha Watanzania nchini humo.
Picha na Kayu Ligopora, Greece