0 0
Read Time:2 Minute, 4 Second

Mhashamu Protase Rugambwa sasa Mhadhama.

KADINALI PROTASE RUGAMBWA

Makardinali wapya watasimikwa rasmi tarehe 30 Septemba 2023.

Makardinali wapya 21 kati yao Makardinali watatu ni wale ambao wamejipambanua katika huduma kwa Kanisa . Makardinali wapya watasimikwa rasmi tarehe 30 Septemba 2023.

Baba Mtakatifu Francisko Dominika tarehe 9 Julai 2023 amewateuwa Makardinali wapya 21 kati yao ni Mhashamu PROTASE RUGAMBWA.

Makardinali wapya watasimikwa rasmi katika mkutano wa kawaida wa Makardinali utakaoadhimishwa tarehe 30 Septemba 2023 mjini Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 13 Aprili 2023 alimteuwa Askofu mkuu Protase Rugambwa kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Tabora, Tanzania.

Makardinali ni washauri wakuu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro

Makardinali ni washauri wakuu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro

Kardinali mteule Rugambwa alizaliwa tarehe 31 Mei 1960 huko Bunena-Bukoba nchini Tanzania, akapata Daraja Takatifu ya Upadri kutoka mikononi mwa Mtakatifu Yohane wa Pili alipotembelea Tanzania tarehe 2 Septemba 1990 na kuwa Padri wa Jimbo Katoliki Rulenge-Ngara. Kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2008 alifanya utume wake kwenye Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu mjini Vatican. Baba Mtakatifu Benedikto XVI, tarehe 18 Januari 2008 akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma, na tarehe 26 Juni 2012 akateuliwa kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari na wakati huo huo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu. Tarehe 9 Novemba 2017 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu. Baada ya kulitumikia Baraza kwa vipindi viwili na muda wake ulipogota ukomo, kadiri ya Katiba mpya ya Kitume inayojulikana kama “Predicate evangelium” yaani “Hubirini Injili” Juu ya Sekretarieti kuu “Curia Romana” na Huduma Yake Kwa Kanisa na Kwa Ulimwengu”

Kardinali mteule Protase Rugambwa akiagana na Papa Francisko mjini Vatican

Kardinali mteule Protase Rugambwa akiagana na Papa Francisko mjini Vatican

Makardinali wapya wanasimikwa tarehe 30 Septemba 2023

Makardinali wapya wanasimikwa tarehe 30 Septemba 2023

Hongera sana Mhashamu Rugambwa.

Balozi wa Tanzania nchini Italy pichani akiwa na Mhadhama Kardinali Protase Rugambwa wakati Maaskofu kutoka Tanzania walipo tembelea Ubalozi wa Tanzania Rome mwezi May mwaka huu. Maaskofu hao walikuwa katika hija maalumu Vatican.

Balozi wa TANZANIA nchini Italy Mh. Mahamoud Thabit Kombo ametoa pongezi nyingi kwa KADINALI RUGAMBWA baada ya taarifa za kuteuliwa kwake.

Mh.balozi amesema uteuzi huu unaendelea kuheshimisha nchi yetu kimataifa. Tanzania imekuwa na historia kubwa na Vatican tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Na katika kumbukumbu kubwa ni pale alipotunukiwa tuzo Sheikh Thabit Kombo Jecha akiwa na Mwalimu Nyerere nchini Vatican. Tuzo hiyo ilitolewa na Papa.

Mkutano huu wa kihistoria ulihudhuriwa na Mhadhama KADINALI PROTASE RUGAMBWA
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %