Rome IT.
WU® MEDIA
Dkt TULIA akisaini kitabu Cha Wageni mara tu alipofika Ubalozi wa Tanzania jijini Rome Italy, pembeni ni mwenyeji wake ambae ni Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh. Mahamoud Thabit Kombo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, aliwasili Jijini Roma Nchini Italia tarehe 22 Julai, 2023 kwa ziara ya kikazi ambapo alipokelewa na Balozi wa Tanzana Nchini humo Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
SPIKA atembelea Ubalozi wa Tanzania Rome
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, jana tarehe 24 Julai, 2023 ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Nchini Italia zilizopo katika Jiji la Roma na kupokelewa na Mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
Katika ziara hiyo ya kikazi Mhe. Dkt. Tulia ameambatana pia na Katibu wa Bunge Bi. Nenelwa Mwihambi ndc, Katibu wa Spika Ndg. Mathew Kileo pamoja na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Bunge.