0 0
Read Time:2 Minute, 0 Second

INTERNATIONAL KARATE SEMINAR

Na Mwandishi wetu

CATANIA, SICILY, ITALY

Kiongozi mkuu wa Chama cha Jundokan  Karate-Do Tanzania (Shibu-cho )sensei Rumadha Fundi pamoja na washiriki wengine 160 toka nchi Zaidi ya 18 katika mabara manne; Ulaya, Marekani kaskazini (Alaska) na kusini (Argentina), Japan (Okinawa), Afrika (Angola na Tanzania), na mashariki ya kati (Israel), Walikusanyika katika kisiwa cha Sicily nchini Italia kwa mafunzo maalum ya chama hicho yanayofanyika kila mwaka ndani ya bara la Ulaya na kuwashirikisha wanachama wenza toka mabara tofauti ikiwemo nchi za Afrika kama Tanzania na Angola

Kongamano hilo huwa na lengo la kuwanoa wakufunzi wa ngazi zote  za mikanda ya karate hususani walimu wa kuu. Jopo la walimu “Masters” toka Naha, Okinawa, Japan visiwa vya chimbuko la karate, huteuwa walimu hao na kuendesha semina hizo.

“Semina hizi za kimataifa hufanywa na mitindo yote ya karate duniani, lakini sasa tunaongelea chama cha Jundokan karate hapa”, alisisitiza sensei Rumadha wakati akiongea na Wabongo Ughaibuni Media….”

Mpaka sasa hivi nimeshiriki semina (Gasshuku) nyingi sana na kwa miaka mingi tokea mwaka 1991 chini ya masters wakubwa toka Okinawa, Japan kama vile Morio Higaonna, Teruo Chinen, Matasaka Muramatsu, Tetsu Gima,Tsuneo Kinjo na Kancho Yoshihiro Miyazato.

“Sidhani kama kuna sensei yeyote Tanzania aliyewahi shiriki semina nyingi na masters wa ngazi za juu kabisa duniani kulingana nami kiukweli”, alisema sensei Rumadha mwenye uzoefu wa karate wa zaidi ya miaka 45 sasa na anashikilia ngazi ya dan 5 aliyopewa na master Yoshihiro Miyazato zaidi ya miaka mitano iliyopita baada ya kufuzu mtihani  toka chama cha Jundokan Karate-do Goju Ryu.

Tanzania, pia imepata mwaliko mwingine kusheherekea miaka 70 ya chama cha Jundokan tangu kianzishwe na mwasisi wake master Eiichi Miyazato 1957 huko Naha, Okinawa ,Japan. Maadhimisho hayo yatafanyika  mwezi Novemba, 2024. Mandeleo ya karate nchini hutegemea sana jinsi gani kila chama kinavyoendeshwa na wakuu wake. Hivyo ipo misingi inayofuata kuhakikisha kila mtindo na vyama vinaendeleza  vipaji vipya vitakavyoendeleza Sanaa hii nchini Tanzania.

Tumepata fursa ya kujifunza mengi na kuzungumza maendeleo na mbinu tofauti za karate. Pia kuweza kukutana na kujuana na walimu (Masensei) toka nchi mbalimbali. “Karate-Do au kwa jina lingine mwenendo wa karate ni kushiriki makongamano kama haya nakuwashirikisha masters wa mitindo yeyote kuhakikisha mbinu hazifuji au kuwa nakutu kimafunzo. Kila sensei huitaji masahihisho toka kwa wenzie wa ngazi za juu kiushirikiano, hivyo ndivyo tunafanya hapa. Sensei Rumadha sasa ameelekea mjini Rome kwa mapumziko kabla ya kurejea marekani.

Happy
Happy
100 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %