0 0
Read Time:38 Second

Paris,France

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amewasili Jijini Paris, Ufaransa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu (3).

Baada ya kuwasili Mhe. Makamba na ujumbe wake aliofatana nao walipata fursa ya kushiriki kikao cha pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Ali Mwadini pamoja na maafisa wa ubalozi huo.

Akiwa nchini Ufaransa Mhe. Makamba atashiriki kongamano la biashara kati ya Tanzania na Ufaransa lililoandaliwa na Shirikisho la Wafanyabiashara wa Ufaransa (Mouvement Des Entreprises De France – International /MEDEF) litakalofanyika tarehe 16 Novemba 2023 jijini Paris.

Vilevile katika nyakati tofauti Mhe. Makamba anatarajia kukutana kwa mazungumzo na viongozi wa Serikali ya Ufaransa pamoja na Wakuu wa Makampuni ya Biashara za kimataifa za nchini humo.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %