
Tel Aviv
Mwili wa Mtanzania aliyeuawa nchini Israel, Marehemu Clemence Mtenga umeagwa usiku huu huko Tel Aviv nchini Israel na ibada yake imehudhuriwa na watanzania kadhaa wakiwemo wenyeji wao.
Kwa mujibu wa taarifa za awali za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mwili huo unatarajiwa kufika nchini Jumamosi hii kwa ajili ya mazishi baada ya Watanzania waliopo Israeli kuuaga mwili huo.
