Mwili wa Diaspora mwenye uraia wa Msumbiji waenda kuzikwa Maputo .
Johanesburg SA
Hatimae mwili wa Ndugu Michael aliyeuwawa kwa kupigiwa risasi nchini South Africa wasafirishwa kuelekea Maputo Msumbiji kwa Mazishi.
Marehemu Mwenye uraia wa Msumbiji alipoteza maisha baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana ingawa kutokana na taarifa kutoka kwa wadau nchini South Africa zilisema kuwa mshukiwa wa tukio hilo ni Mtanzania mwenzie ambae walikuwa wakidaiana pesa. Michael alikwenda South Africa katika huo mchakato wa kudai haki yake ndipo yalipomfika mauti. Mtuhumiwa inasemekana amekamatwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania huko amekuwa akifuatilia kwa karibu sana tukio zima tangu Marehemu alipouawa. Baada ya mchakato wa kupata mwili wa marehemu kuikamilika ndipo safari ya kuusafirisha mwili ikaanza kuelekea Maputo Msumbiji. Katika taarifa yake Ndugu Msangi ambae ni Mwenyekiti wa Watanzania ameonekana pichani akiwa na mwili wa marehemu kwenye gari maalumu kwa ajili ya kusafirisha mwili. Michael au Mike aliuawa kwa kupigwa risasi sehemu inayoitwa Taxi Rank Twist/ Plain Jijini Johannesburg, South Africa . Pamoja na mauaji hayo lakini inasemekana maeneo hayo ya Taxi Rank yamekuwa na mauaji ya kutisha na kuwa ni eneo hatarishi kwa ujumla.
Mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea Msumbiji ambako ndiko kuna familia yake, Marehemu ameacha mke na watoto.
Mwili wa marehemu Michael wawasili Msumbiji kwa mazishi
Marehemu Michael amekwisha zikwa, Mola ailaze roho yake mahala pema. “Wabongo ughaibuni Media inaungana na Watanzania South Africa, ndugu jamaa ,marafiki na familia ya marehemu katika kuomboleza msiba huu.”
Taarifa na Picha kwa hisani ya ndugu
Mohamed Msangi