0 0
Read Time:1 Minute, 31 Second

Ziara ya Waziri wa Mambo ya nje wa Hungary nchini TANZANIA

Tanzania imesainia Mkataba wa Ushirikiano na Nchi ya Hungary katika sekta ya maji ili kubadilishana uzoefu wa teknolojia katika sekta hiyo.

Akizungumza leo Machi 28,2024 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Janury Makamba amesema kwa miaka mingi nchi hiyo inaongoza kwa teknolojia ya juu Duniani katika udhibiti wa maji ikiwemo maji taka,mafuriko na ya kunywa hivyo ushirikiano huo wa karibu utaleta tija kubwa kwa Taifa .

Sambamba na hayo amesema nchi hizi mbili zimekuwa zikifanya biashara hivyo kutafanyika makongamano ya kibiashara ili fursa zilizopo zinufaishe pande zote.

“Tanzania ina vivutio vingi vya utalii na Hungary ni chanzo cha watalii kwani tumeshuhudia watalii wengi kutoka nchi hiyo wakija kutalii na miaka iliyopita walikuwa 5000 mwaka jana wakifikia 11000 hivyo kuna ongezeko kubwa kutoka nchi hiyo na kwa kuona hilo tumezungumza kwa kina na kujubaliana kuwa tutasaini usafiri wa anga watalii na wafanya biashara watatoka moja kwa moja kutoka Hungary kuja Tanzania kwa ndege”Amesema Makamba

Pamoja na hayo pia amebainisha kuwa Vijana wa kitanzania wamekuwa wakinufaika kwa kupata ufadhili wa kwenda kusoma Hungary pia wamekubalina kunzisha mahusiano ya kituo cha Diplomasi cha kimataifa cha Dkt Salim Ahmed Salimna na chuo cha Diplomasia ambapo itasaidia wanadiplomasia kupata fursa ya kwenda Hungari kuongeza ujuzi.

Waziri Makamba amesema nchi ya Hungary wamedhamiria kuwekeza kwenye kiwanda cha kutengeneza ndege ndogo Morogoro.

Aidha nchi ya Hungary imekubali kujenga Ubalozi wao nchi Tanzania uliofungwa miaka ya 1990″ hiyo ni moja ya kusaidia kuongeza mashirikiano makubwa baina ya nchi hizo mbili.

Naye Waziri wa Mambo ya nje na Biashara wa Hungary Mhe Peter Szijj’art’o amesema licha ya kufungwa kwa ubalozi lakini bado ushirikiano ulikuwa unaendelea hivyo habari njema ni kuwa nchi yao mwaka huu mwezi wa saba inatarajiwa kuchukua Urais wa Umoja wa Ulaya.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %