0 0
Read Time:55 Second

London UK

Bank ya NMB ya Tanzania imekuwa bank ya kwanza Afrika ya mashariki kusajili Sustainability Bond katika soko la hisa la London Uingereza. Katika tukio hilo muhimu serikali iliwakilishwa na Balozi wa Tanzania UK Mh. Mbelwa Kairuki.

“Ninaipongeza Benki ya NMB Tanzania kwa tukio la leo la kusajili Jamii Bond katika soko la Hisa la London LSEplc .” ….Alisema Mh Balozi , Benki hiyo imeweka historia kwa kuwa ya kwanza kutoka nchi za Afrika Mashariki kusajili Sustainability Bond katika Soko la Hisa la London. Tukio hili maana yake Benki ya NMB inaaminika kimataifa, na mazingira ya uchumi ya Tanzania yanatia matumaini katika masoko ya Kimataifa kutokana na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pia Mh Balozi amempongeza sana Mkurugenzi Mkuu wa NMB Bi Ruth Zaipuna na timu yake kwa kufungua njia. Kwa jitihada zinazoendelea, bila shaka tutashuhudia Makampuni mengine ya Tanzania yakiingia katika anga za kimataifa kutafuta mitaji kupitia Soko la Hisa la London.

Don’t forget to subscribe to our YouTube Channel

WABONGO UGHAIBUNI MEDIA
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %