Na GFAMILY KAGUTTA
WU®MEDIA, ITALY
Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi Mbalimbali. Katika taarifa iliyotolewa na katibu mkuu Kiongozi, Balozi Dkt Moses Kusiluka pia Rais amemteua Kuwa Mbunge na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, Mh. Mahmoud Thabit Kombo ,ambae kabla ya uteuzi alikuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy . Balozi Mahmoud Thabit Kombo anachukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo Mh. January Yusuf Makamba (MB) ambae uteuzi wake umetenguliwa Jana.
Mh. Balozi Mahmoud Thabit Kombo Katika kazi zake kwenye kituo cha Rome Italy pia alikuwa anawakilisha Italy,Croatia, Greece, Slovenia, Macedonia, Albania, Bosnia- Herzegovina, Serbia, Malta Montenegro, FAO, IFAD and WFP.