0 0
Read Time:31 Second

Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU-PSC) ngazi ya Wakuu wa Nchi kujadili hali ya usalama nchini Sudan.

Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, chini ya Uenyekiti wa Baraza hilo kwa mwezi Juni 2024, Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Tanzania imeeleza kusikitishwa na mapigano nchini humo. Aidha, Tanzania imeungana na nchi nyingine kukemea vikali mauaji yanayoendelea nchini Sudan dhidi ya raia wasio na hatia.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %