11/06/2024, SWISS
Balozi wa Tanzania Mh. Hassani Iddi Mwamweta leo amewasilisha Hati za Utambulisho (letters of Credence) kwa Mheshimiwa Viola Amherd, Rais wa Shirikisho la Uswisi.
Pamoja na kuwasilisha salamu za upendo kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi pia alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Uswiss kwa namna inavyoshirikiana kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania.
Mh Balozi alitumia fursa hiyo pia kuomba ushirikiano zaidi na Serikali ya Uswiss kwenye maeneo ya vipaumbele ambavyo ni pamoja na utalii; biashara na Uwekezaji; elimu na afya.
Balozi pia alimshukuru kwa mchango wa Serikali yake kwenye jitihada za kuboresha amani na Usalama kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu.
Mahusiano baina ya Tanzania na Uswisi ni mazuri na ya kihistoria. Pamoja na Uswisi Mh. Hassan Iddi Mwamweta ni balozi anaewakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani, Poland, Holy See (VATICAN), Czech, Slovakia, Burgaria, Romania na Hungry.