0 0
Read Time:2 Minute, 1 Second

Na GFAMILY KAGUTTA

Mashindano makubwa ya soko barani Ulaya yanayojumuisha timu za diaspora za Tanzania Ughaibuni kwa mwaka 2024 yamehitimishwa jana jijini The Hague nchini Netherlands.

Mashindano hayo yanayojulikana kama Serengeti Football Bonanza yalihudhuriwa na Mwenyeji na mlezi wa Mashindano hayo Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania The Hague, Mh. Caroline Kitana Chipeta na Mh. Jestas Abuok Nyamanga Balozi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ubelgiji.

H.E. Ambassador Caroline Kitana Chipeta
Ambassador Extraordinary and Plenipotentiary & Permanent Representative to the OPCW

Ambassador of the United Republic of Tanzania to the Kingdom of Belgium, Grand Duchy of Luxembourg and the Head of Mission to the European Union. He is also the Head of Mission to the Organisation of the African, Caribbean and Pacific States (OACPS) and the Representative of the United Republic of Tanzania to the World Customs Organisation (WCO)

Serengeti Football Bonanza kwa mwaka huu 2024 zilishiriki timu za Diaspora kutoka Uingereza,Germany, Sweden, Belgium na Netherlands. Mashindano hayo yaliyochukua muda wa siku mbili yalikuwa na upinzani mkubwa kulinganisha na miaka iliyopita.

Mechi ya fainali ilikuwa kati ya Mabingwa watetezi Kilimanjaro FF ya Sweden na Serengeti ya Belgium ambapo mpaka kipyenga cha mwisho matokeo yalikuwa bilabila huku Kilimanjaro wakicheza kumi uwanjani baada ya mchezi wao kupewa kadi nyekundu. Ushindi wa Kilimanjaro FF ulipatikana kwa penati Kwa kuitoa Serengeti ya Belgium wa matokeo ya (4 -3 )ambayo ilikuwa ikipata ushauri wa kifundi kutoka kwa mchezaji mkongwe wa Tanzania Jamhuri Kiwelu (JULIO) ambae alihudhuria mashindano hayo.

Mashindano hayo pia yalihudhuriwa na Mbunge wa viti maalumu Mh. Neema Rugangira ambae ni mdau mkubwa wa Diaspora. Mh Rugangira alipokuwa akiongea na Mwenyekiti wa Kilimanjaro FF wakati mashindano yakiendelea, alipongeza jitihada zinazofanywa na Diaspora na kuungwa mkono na balozi za Tanzania hasa katika kuandaa mashindano hayo yanayotoa fursa kwa diaspora kukutana, kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia michezo. Katika mashindano hayo pia Diaspora wanakutana na fursa mbalimbali kama ilivyokuwa mwaka huu kupitia wadhamini wakuu Bank ya NBC ambayo ilitoa huduma kwa diaspora kufungua akaunti za akiba nyumbani.

Wakati wa kufunga mashindano Mh balozi Chipeta, aliwapongeza Diaspora wote kwa kuhudhuria na kushiriki mashindano hayo ambayo ni fursa kubwa ambayo itaendelea kukua kila mwaka. Mh Balozi pia aliwashukuru wadau wote wadhamini wa mashindano.

Kilimanjaro FF ni timu ya Kitanzania ilisajiliwa nchini Sweden na inashiriki ligi ya daraja la sita

Msimamo wa ligi daraja la sita Sweden ambako Timu ya Kilimanjaro inashiriki
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %