
Dar Es Salaam

Tanzania na Ireland zimekubaliana kukuza maeneo ya ushirikiano katika diplomasia ya uchumi.
Katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, jijini Dar es Salaam, Mhe. Balozi John Ulanga, Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, amefanya mazungumzo na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Nicola Brennan na kujadili baadhi ya maeneo ya kipaumbele.
Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja Uchumi wa kidijitali ikiwa ni hatua katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali Tanzania 2024-2034, uwekezaji, teknolojia na ubunifu, kubadilishana ujuzi na biashara katika kilimo cha bustani.
Kwa upande wake Balozi Brennan ametumia fursa hiyo kuelezea kuhusu Kongamano lijalo la kiuchumi kati ya Ireland na nchi za Afrika (Afrika Ireland Economic Forum) lililopangwa kufanyika Juni 2025, jijini Dublin nchini Ireland.
