TANZANIAN DIASPORA IN EGYPT
TAARIFA YA SHUKRANI
Uongozi wa Tanzania Diaspora in Egypt ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Zaituni Nassoro Abdallah unapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri chini ya Mhe. Meja Jenerali Richard Mutayoba Makonzo kwa kufanikisha Uchaguzi wa Viongozi wa Wanadiaspora Nchini Misri uliofanyika jana tarehe 27/9/2024 Nyumbani kwa Balozi.
Pia kwa dhati Uongozi unapenda kutoa shukrani za kipekee kwa Watanzania na Wanadiaspora wote tuliohudhuria katika Uchaguzi na kuweza kufanikisha kuwachagua viongozi wetu Mungu awabariki sana na tunatarajia Umoja, Upendo na Mshikamano katika kuyaendea yale yote yenye Maslahi na Tanzania na Watanzania waishio Nchini Misri.
Pia tunapenda tena kuhimiza ushirikiano baina yetu Viongozi wa Wanadiaspora na Wanadiaspora katika kujenga na kuimarisha Umoja huu na katika hilo wafuatao ni Viongozi wa Umoja wetu.
UONGOZI WA TANZANIAN DIASPORA IN EGYPT
MWENYEKITI
Mhe. Zaituni Nassoro Abdallah
KATIBU MKUU
Mhe. Khamis Mustafa Kandi
KATIBU FEDHA
Mhe. Mariana John Kuzilwa
KATIBU JAMII
Mhe. Hussain Said Shamte
KATIBU MICHEZO
Mhe. Ibrahim Haji Khamis
Asanteni sana!
“Umoja, Amani na Upendo”
Imetolewa na:
Uongozi wa Tanzanian Diaspora in Egypt