
Istanbul TURKEY
UEFA Friendship Cup 2025
Tarehe 02 Aprili 2025, Mhe. Iddi Seif Bakari, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki, ameitembelea Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17 (U17), “Serengeti Girls” ambayo inashiriki Mashindano ya Kimataifa ya Kirafiki ya UEFA Friendship Cup 2025 yanayofanyika Istanbul, Uturuki.
Timu hiyo ilicheza mchezo wake wa kwanza tarehe 31 Machi 2025 dhidi ya Lebanon ambapo ilishinda goli 1- 0, na tarehe 03 Aprili 2025, itacheza mchezo wake wa pili na Jamaica. Mashindano hayo yanajumuisha jumla ya timu nane (8) kutoka Tanzania, Zambia, Uturuki, Colombia, Thailand, Finland, Lebanon na Jamaica na yatafikia kilele tarehe 10 Aprili 2025.
Kwa upande wake Balozi ameipongeza timu hiyo kwa kushiriki katika mashindano hayo na kuanza vema, ambapo ameihakikishia ushirikiano wakati wote wa mashindano. Aidha, ameitakia Timu hiyo heri na mafanikio katika michezo inayofuata ili kuipeperusha vema bendera ya Tanzania kimataifa na kudumisha diplomasia ya michezo

