0 0
Read Time:1 Minute, 7 Second

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamadi Yussuf Masauni amesema wakati Tanzania ikiendelea kutatua changamoto za upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia, Serikali inaongeza juhudi za ushirikiano wa kimataifa na kikanda ili kuondokana na vikwazo katika maeneo mbalimbali kama vile Mipango ya Kujenga Uwezo na Uhamasishaji, Utafiti, Ubunifu, na Maendeleo ya Teknolojia, Msaada wa Kifedha na Kiufundi, Ufuatiliaji, Tathmini, na Tathmini ya Athari.

Ameyasema hayo Machi 28, 2025 jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na balozi wa Finland nchini Tanzania Mhe. Balozi Theresa Zitting, Balozi wa Korea nchini Tanzania Mhe. Balozi Bi. Ahn Eunju pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Balozi Marianne Young.

Mhe. Masauni amekutana na viongozi hao jijini Dar es Salaam Machi 28, 2025 ambapo amesema Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR) inakaribisha ushirikiano na wadau katika maeneo muhimu kama vile Mipango ya Mabadiliko ya Tabianchi na Kusaidia Utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupika (2024–2034).

“Ofisi ya Makamu wa Rais inahusika na masuala mawili, moja ni Uratibu wa Mambo ya Muungano, kwani utakumbuka kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili (Tanganyika na Zanzibar). Ofisi hii pia ina jukumu la uangalizi wa kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mazingira na sheria, mikakati na vyombo vingine vya sera husika.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %