0 0
Read Time:54 Second

Rais Samia atua Luanda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Luanda, Jamhuri ya Angola kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu iliyoa tarehe 7 hadi 9 Aprili 2025. Ziara hii inafanyika kufuatia mwaliko rasmi wa Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe.João Manuel Gonçalves Lourenço.

Lengo kuu la ziara hii ni kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kimkakati kati ya Tanzania na Angola.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 de Fevereiro, Rais Samia amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe.Tete António akiambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo. Viongozi wengine waliokuwapo ni Balozi wa Tanzania nchini Angola mwenye Makazi yake nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Sandro de Oliveira pamoja na viongozi wengine wa serikali.

Ziara hii ni ya kihistoria, kwani ni mara ya kwanza kwa Rais wa Tanzania kutembelea Angola katika kipindi cha miaka 19, tangu ziara ya mwisho ya Rais Mstaafu, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa madarakani mwaka 2006.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %