0 0
Read Time:2 Minute, 48 Second

WATANZANIA TUMELOGWA AU HATUJALOGWA?

Na Thadei Ole Mushi.

Serikali imesema inatumia sh Bilioni 22 kuagiza Maziwa nje ya nchi. Hii ni Hatari kabisa….

Juzi Juzi niliwaandika hapa kuwa:-

Jarida la Xinhua 2019 liliripoti kuwa viwanda 15 vya Maziwa viliweza kufunguliwa nchini TANZANIA baada ya Serikali kuzuia uingizaji wa Bidhaa za Maziwa hovyo hovyo.

Kwenye habari hiyo inamtaja Sophia Mlote Msajili wa TDB (Tanzania Dairies Board) ambaye anasema viwanda hivi vipya 15 vina uwezo wa kuzalisha Lita za Maziwa 94, 400 kwa siku.

Yaani viwanda 15 vinazalisha Lita chini ya laki Moja kwa siku huku Bidhaa nyingi za Maziwa kama Milk powder Tanzania ikiwa haiwezi kuzalisha.

Fuata link kusoma habari hiyo http://is.gd/3w4tJf

Wakati viwanda 15 vikishindwa kufikisha Lita laki Moja kwa Tanzania wenzetu Kenya kiwanda kimoja Cha Brookside kwa siku Wana uwezo wa kuzalisha lita 1.5 million. Yaani kiwanda kimoja kinazalisha mara Tano zaidi ya viwanda 15 vya Tanzania.

Brookside ni Moja ya kiwanda kikubwa Cha Maziwa pale Kenya vipo vya Aina hiyo zaidi ya 15 ambavyo Maziwa yanayotokana na Ng’ombe wao hayatoshi hivyo hulazimika kuvuka Mipaka kutafuta Raw material ya Maziwa. Tuliwahi kuwazuia pale Arusha 2005 Brookside wasinunue Maziwa yetu lakini baada ya wao kuondoka Bei ya Maziwa ilishuka Sana watu wakaenda kwa Mh Pinda kuomba Wakenya waruhusiwe kununua Maziwa. http://is.gd/AqTvqb unaweza kupitia link hiyo kusoma sekeseke Hilo.

Brookside pekee inaweza kulisha Maziwa nchi nzima na kwa kuwa tunayapata toka kwao na kwa Bei rahisi basi kiwanda hiki pekee kinaweza kuua viwanda vyetu vyote vya Maziwa nchini.

Kwa wale ambao hawajui ni kwamba Tanzania ni nchi ya nne Africa kuwa na mifugo mingi nyuma ya Somali, Sudani na Ethiopia. Zaidi ya asilimia 50 ya wakazi wake wanajishughulisha na Ufugaji… Hivyo kama tutaweza kuwekeza hapa vizuri tutafungua kaya nyingi Sana Maskini na tunaweza kuzalisha ajira za kutosha za vijana wetu ambao hawana Ajira.

Dr Mayasa Simba Meneja wa TDB aliwahi kusema kuwa uwezo wa Tanzania kuzalisha Maziwa ni asilimia 40 tu. Asilimia nyingine 60 tunaagiza nje ya nchi. Tunashika nafasi ya nne kwa Mifugo mingi Ila tunaliashwa Maziwa na nchi ambazo hata kwenye kumi Bora ya kuwa na mifugo mingi hawapo.

Kinachofanyika kwa sasa ni Kuwa Tanzania inabakia kuwa hub ya Raw materials tu ambayo kimsingi haina faida yoyote kama hatutaongeza thamani ya mazao yetu. Hata haya mahindi tukiyasaga tu na kuyauza kama unga tutazalisha ajira za kutosha na tutapiga hela ya maana Sana. Kama kweli wanatupenda waturuhusi tuuze Unga wetu kwao badala ya mahindi. Kwa nn tunashindwa bado sielewi…. sijui kwa nn tunacheza na Ufugaji ni eneo muhimu sana kwa ustawi wa Taifa Hili….

Rwanda kwa kufahamu umuhimu wa kuondoa umaskini kwa Kutumia tu Mifugo kila familia Maskini nchini Rwanda imegawiwa Ng’ombe mmoja wa Maziwa katika sera yao inayoitwa “Girinka” Sisi bado tumelala.

Achana na haya Maziwa…. Njoo kwenye Issue ya mafuta ya kula. Mwaka 2019 tulitumia zaidi ya bilioni 400 kuagiza mafuta nje ya nchi. Tuna Ardhi yenye Rutuba, tuna maji kila pembe ya nchi hii, tunalima Michikichi, Pamba, Alizeti nk lakini tuna uwezo wa asilimia 40 tu wa kuzalisha mafuta nchini asilimia 60 tunaagiza nje ya nchi.

Link hii inaonyesha kiasi Cha mafuta tulichoagiza 2019.

https://www.itv.co.tz/news/tanzania-yatumia-bilioni-400-ikiagiza-mafuta-ya-kula-toka-nje

Tutatengenzaje ajira kwa watu wetu kwenye thinking ya Aina hii? Tuendelee kuwaambia madereva wawashe AC kwenye V8 zetu…

Ole Mushi
0712702602.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %