0 0
Read Time:4 Minute, 11 Second

BURIANI KATIE KAHN CARL

Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mama Katie Kahn Carl. Allah amfanyie wepesi mama huyu mmoja kati ya family friends wangu.

Je Katie ni Nani?

Katie ni Mtoto wa Mzee Kahn Carl ambaye ndiye alijenga MARANGU HOTEL. Mzee Kahn allikuwa mzaliwa wa Austria na alikuwa kwenye orodha ya wahanga wa Hitler. Alipoona anasakwa akakimbilia Ireland kujificha. Kipindi hicho Ireland vichaka na nyumba chache! Alipofika Ireland akaoa na kuzaa watoto wawili Katie na Lucie. Bado majasusi ya Hitler yakamfuatilia. Alipoona atakamatwa akaondoka na meli kwenda nchi inaitwa Tanganyika. Alipomuona Julius Nyerere nyakati za harakati za uhuru akamshauri ni vyema akaishi Marangu. Pamejificha na hali ya hewa haitamsumbua. Na utawala wa Gavana wa Kiingereza ukamsaidia vijisenti. Mzee Kahn ikamlazimu kuomba kazi. Akaomba KNCU na TPC LTD. Kote wakamkubalia lakini akachagua TPC. Enzi hizo TPC mali ya mfalme wa DENMARK. Akaajiriwa kama AFISA UTAWALA. Ndiye afisa utawala wa kwanza TPC. Kutokana na mateso aliyopitia akaamua kuanzisha tawi la Chama Cha wafanyakazi pale TPC. Huenda lilikuwa kati ya matawi ya kwanza kabisa ya Chama Cha wafanyakazi nchini! Alifanya hivyo baada ya kushauriana na Marehemu Mzee VICTOR MKELO aliyekua kiongozi wa Chama Cha wafanyakazi wa mkonge Tanzania. Nafarijika nilishiriki kumjengea Nyumba Mzee Mkello mwaka 2001. Tulimtembelea na kumkuta anaishi vibaya mno. Hakuna aliye muenzi Mzee Mkello. Mzee aliyeendesha mapambano ya kutetea wafanyakazi wa mkonge (manamba) Tanzania.

Turudi kwa mzee Kahn.

Mzee Kahn aliamua kujenga hôtel. Ndio MARANGU HOTEL. Enzi zile hoteli zilikuwa 2 tu Kilimanjaro. Livingstone (sasa Moshi Hôtel) na MARANGU HOTEL!

Mzee Kahn ndiye alimshawishi Dr. Baleto kufungua clinic pale Marangu. Enzo zile ukawa Kila mgonjwa lazima apelekwe KWA BALETO papaangu! Kupata chanjo, kutahiriwa, kudungwa sindano n.k. Usipopelekwa KWA BALETO utapelekea Moshi mjini KWA DOKTA MORTALLA. Huyu alikuwa mhindi. Ni huyu Kahn alishiriki vizuri kuanzia Middle School pale Katanini na kule Mwika. Alitoka kipaumbele sana kwa Elimu na Afya.

Watoto wa Mzee Kahn – Marehemu Katie na Lucie walikuja wakiwa wasichana kama WA mipaka 15-18 hivi. Wakichanganyika mnoo na dada zetu. Mimi nilikuwa MDOGO mnoo kipindi hicho. Ila nakumbuka baisikeli Zao. Ndio peke walikuwa na baisikeli! Wengine woote baisikeli za mbao. Basi wakiachia wenzao wa umri wao waziendeshe. Haswa kutoka Marangu Mtoni kuja Marangu Katanini mpaka Himo. Zikichakaa wanaletewa mpya lifti zinaanzaa upyaaa. Nakumbuka dada zangu n’a hizo baisikeli.

Mabinti hawa walirudishwa Ireland nadhani mwaka wa 1964 (kama sikosei kuanza vyuo. Mdogo ambaye ni Luci) alienda kujiunga na Loreto Collège (kunazo branch Tanzania na Kenya) na Katie alijiunga CHUO kikuu Cha Dublin (UCD) CHUO ambacho nami nilisoma shahada ya uzamili. Kuondoka kwao kulituletea majonzi watoto. Lifti za baisikeli, biskuti, Keki, chokoleti zikaisha! Hakika hakuna aliyedhani atakuja kuonana nao tena.
Sherehe ya kuwaaga illikuwa na kawimbo “gudu Bai, gudu baiii, you are going away, we are very sorry you are going away we shall meet again, when we meet again…..”! Watoto wa kichaga sasa hapo utachekaaaa!

Baadaye Mzee Kahn naye akaamua kurudi kwao Austria. Lakini mzee Kahn hakusahau wema wa Tanzania! Kabla hajaondoka alimfuata Julius Nyerere na kumpa Hôtel bureee kama shukrani ya ukarimu na usalama aliopewa na Tanzania! Mwalimu akaikabidhi hotel kwa shirika la utalii Tanzania (TTC)! Ndio MARANGU HOTEL ambayo nadhani ilikuja kuuzwa!

Mungu si Joni wala Salèhe! Siku moja nikiwa Dublin niliambatana n’a Mwalimu. Wamisionari wakatoliki wakaandaa chakula cha jioni. Wakati wa chakula akanijia mama mmoja na kunisalimia “shimbonyi”! Nikamuitikia “namchicha” 🤣. Wote tukakumbukana! Mama allikuwa na picha zetu na mie nilikuwa na picha zao! Japo nilikuwa mdogo kwake hatukusahauliana. Walikuwa marafiki sana wa baba. Mara kadhaa tukienda kulala kwao nao wakija kulala kwetu pale Himo. Wakipiga makande na kishumba île mbaya! Masikini dada zangu Amina na Fatuma waliokuwa umri wao walishafariki. Alilia sana nilipomjulisha mpaka Mwalimu akamuuliza kulikoni? Mama akamkumbusha yéyé ni nani!

Basi nilipoenda kusoma Dublin alinipokea kama mdogo wake. Hakika ndiye alichakarika Nipsey scholarship Toka kwa Mama Mary Robinson.

Niliishi kwake kwa raha mustarehe. Katie alipomaliza chuo alipata kazi RTE (Television Ireland) ambapo alipanda hadi kuwa Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari za Kimataifa. Ni kupitia yéyé niliweza kuingia studio kuubwa kabisa kuona inavyoaandaa vipindi mbalimbali. Siku ananitembeza studio illikuwa inaandaa kipindi maarufu kikiitwa FATHER TEDDY. Kikipendwa sana Ulaya. Kilikuwa comedy kuhusu mapadre kanisa katoliki. Alifanya uanafunzi wangu uwe wa raha.

Baadae Lucie na Katie walikuja kunitembelea nyumbani Tanzania mara 2. Na mara zoote tukienda Marangu na Himo kuwaona waliocheza nao utotoni. Na waliokuwa wafanyakazi nyumbani kwao na hotelini kwao. Wakiwaletea zawadi kedekede! Pia hawakuacha kutembelea TPC na Loreto Girls Mwanza.

Mama Katie alikuwa na zawadi spesheli kwangu na familia kila Xmas! Xmas haipiti bila card na euro! Hâta nikimwbia Kadi inatosha anajibu “hakuna Siku héla inatosha maana kuna ndugu wengi wanazihitaji”!!!

Mdogo wake Lucie ndiye alinipa taarifa hizi kwa simu jana. Kwa sasa anaishi kusini mwa France. Naye hataweza kuhudhuria mazishi kutokana na zuio litokanalo na covid.

Katie atazikwa Jumatano ijayo. Kwa heshima yake RTE wataonyesha mazishi yake live kupitia link maalumu na kwa watu waliochaguliwa na Katie mwenyewe kwenye wosia wake. Na mie nimo!

Kwaheri Katie WE SHALL MEET AGAIN. YOU WERE A HUMAN BEING WORTHY KNOWING AND BEFRIENDING

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %