0 0
Read Time:2 Minute, 43 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba,2021
.

Rais mmoja wapo wa Nchi ya Marekani aliwahi kusema kwa lengo la kuwakumbusha wa Marekani wajibu wao kwa Taifa lao kwa kusema,Nanukuu”…..usijiulize kwamba Marekani imekufanyia nini hila jiulize umeifanyia nini Marekani…..”.My fellow Americans: Ask not what your country can do for you – ask what you can do for your country.” John F Kennedy.

Kauli hii hata baada ya miaka mingi kupita bado inabeba uzito mkubwa katika maisha ya vijana wa Leo wa kitanzania kwani ni lazima kila Kijana wa kitanzania alipo ajaribu kujiuliza je,nii kwa kiasi amewajibika kwa Tanzania ili kuweza kufikia ustawi wa Taifa pamoja!

Vijana wa kitanzania regardless ya tofauti zetu za kimtazamo lakini bado tunaendelea kuunganishwa na utanzania wetu na kamwe hakuna kinachoweza kutupokonya utanzania wetu!

Wajibu wetu kwa Tanzania yetu haupaswi kutikisika wakati wowote na mtu yoyote,kwahiyo tuna wajibu mkubwa wa kuuwimba wimbo huu kwa maslahi ya Tanzania ya Leo na Kesho,kwa maslahi ya vizazi vya Leo na Kesho!Hivyo basi vijana wa kitanzania tunapaswa kuyaishi haya;

1.Nina imani katika Taifa langu la Tanzania,imani yangu ni kwamba,Tanzania tunaweza kuwa Taifa bora duniani tukifanya kazi kwa bidhii na maarifa!

2.Sisi vijana wa kitanzania tutakuwa mfano wa Uadilifu,utiii na uzalendo kwa kuanzia kwenye familia zetu mpaka Taif ili kuweza kutimiza malengo ya pamoja ya Taifa kabla ya kutimiza malengo yetu binafsi.

3.Vijana wa kitanzania tutachukia rushwa,ubinafsi,wizi,uzembe na tutajitoa kulitumikia Taifa letu kupitia elimu zetu,maarifa yetu,imani zetu kwa maslahi ya Watanzania wote.

4.Kila mara vijana wa kitanzania tutasisitiza na kuuishi umoja wa kitaifa,undugu na tutaukataa ukabila,udini,ukanda,matabaka kwa lengo la kudumisha mshikamano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

5.Vijana tutajitoa kutetea maslahi ya Tanzania mpaka tone la mwisho la damu kwa ajili ya kulinda Uhuru wa mipaka ya Taifa letu,kulinda maslahi ya kiuchumi ya Tanzania pamoja na maslahi ya tamaduni zetu.

6.Vijana hatutothubutu kuisema vibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wake wa sasa na wastaafu kwa lengo la kulinda heshima na sura njema ya Taifa letu la Tanzania.

  1. Vijana tutawajibika kuliombea Taifa na viongozi wake kwa imani zetu kabla ya kufanya maombi yetu binafsi.

8.Vijana tutajitoa kwa kadri ya uwezo wetu na kila siku tutawaza ni kitu gani chema tuiifanyie Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watu wake kwa ajili ya ustawi wa Taifa.

9.Vijana tutakuwa na heshima kwa watu wa rika zote na kulinda maadili na utamaduni wa Taifa kwa vitendo kwa kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia,ukatiri kwa watoto na kulinda haki za walemavu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

10.Vijana tutakuwa wasemaji hodari wa mafanikio na maono ya Taifa letu popote tutajapokuwa ndani na Nje ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tutajitaidi kujivunia Nchi yetu katika viwango vya juu kabisa.

Vijana wa kitanzania tukishafikia hapo basi ni wazi kuwa tutakuwa tumejenga Taifa imara zaidi kwa ajili ya vizazi vijavyo!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani Serikali ya wanafunzi Daruso-IJMC,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli,Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Saut & University of Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255746726484
+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %