0 0
Read Time:1 Minute, 39 Second

Tuzo ya Nobel

Na Abbas Mwalimu (0719258484).

Ijumaa tarehe 8 Oktoba, 2021.

Nimefuatilia mijadala mingi ya tangu jana baada ya Bwana Abdulrazak Gurnah kutwaa tuzo ya Fasihi ya Nobel.

Mjadala mkubwa upo kwenye uraia na utaifa wake.

Nadhani kuna dhana mbili ambazo wengi tunashindwa kuzing’amua, dhana hizi ni Citizenship vs Nationality ama Uraia dhidi ya Utaifa.

Mtu anaweza asiwe raia wa nchi fulani lakini ana utaifa wa nchi fulani.

Uraia unaweza kufa au kubadilishwa lakini utaifa haufi wala kubadilishwa.

Uraia unatolewa na nchi lakini utaifa ni kule alikozaliwa mtu au wazazi wake.

Kwa mfano, wakurdi ni taifa lenye watu zaidi ya milioni 6 duniani,hawa hawana nchi yao lakini ni taifa ambalo limetawanyika katika nchi za Uturuki, Iran, Syria na Iraq.

Hivyo kuna wakurdi raia wa Uturuki, kuna wakurdi raia wa Iran, wengine ni raia wa Syria na wengine wa Iraq

Hivyo kwa muktadha huo ni sahihi kwa Bwana Abdulrazak Gurnah kuitwa Mtanzania mwenye uraia wa Uingereza kama ambavyo vyombo vingi vya nje vimemtambulisha.

Kwa nini Mtanzania?

Kwa sababu ni Mzanzibari na Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyobainishwa kwenye ibara ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sambamna na marekebisho yake mbalimbali:

  1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

Lakini pia tusome ibara ya 6 (1) katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010 kuhusu nani ni Mzanzibari

6.-(1) Kutakuwa na Mzanzibari ambaye upatikanaji wake, upoteaji wake na urudishwaji wake atakuwa kama alivyoainishwa katika sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Lakini tusome pia ibara ya 2 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sambamba na marekebisho yake yote.

2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na nipamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzaniainapakana nayo.

Hivyo Abdulrazak Gurnah ni Mtanzania mwenye Uraia wa Uingereza.

Wenu:

Abbas Mwalimu
(Facebook|Instagram|Twitter|Clubhouse)

+255 719 258 484

Uwanja wa Diplomasia
(Facebook|WhatsApp).

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %