0 0
Read Time:4 Minute, 43 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.

Hata ingetokea ningekuwa jiji Dar es salaam kwa siku ya kesho ambayo Nchi yangu nzuri Tanzania itakuwa inatimiza miaka sitini ya uhuru wake bado isingetosha kunisogeza uwanja wa Taifa kuungana na RAIS wangu kipenzi Mh Samia SULUHU HASSAN pamoja,Watanzania pamoja na wanaccm wenzangu huku tukijipongeza kwa kutimiza miaka sitini ya uhuru!

Baba wa Taifa 1961

Sio kwamba nataka kubeza mafanikio yetu kama NCHI ndani ya miaka sitini ya uhuru wetu lakini mimi kama Kijana ninaona wazi kabisa Taifa hili halipaswi au halikupaswa kuwa hapa lilipo baada ya miaka sitini ya uhuru wetu!Vijana wa NCHI hii hatupaswi kuwa na mawazo ya kimasikini masikini kwani tukifanya hivyo hatutalifikisha kwa wakati Taifa hili linapotakiwa kufika!

Kesho uwenda ndio ikawa siku yangu nzuri ya kujifungia ndani na kufanya tafakuri ya kina ya nini kimetufanya kuwa hapa tulipo mpaka leo kama Taifa wakati mataifa mengine yameenda hatua kubwa zaidi mbele yetu.Nahitaji kuwa na majibu ya maswali haya kwani kwangu kufanya hivyo ndio naona ni njia bora ya kuutafuta uhuru wa NCHI yangu kwa mara ya pili toka kwa “mabeberu”.

SHEREHE ZANGU ZA MIAKA SITINI YA UHURU ZINGEANZIA HAPA!

Mwaka 1990 GDP kwa maana ya pato la Taifa ya Nchi ya Vietnam ilikuwa sawa (6.472 Billion USD) au karibu sana na Tanzania ambayo kwa mwaka yaani 1990 huo huo ilikuwa na GDP ya (4.259 Billion USD).Mwaka wa 2020,GDP ya Nchi ya Vietnam imefikia(271.2 Billion USD) wakati Tanzania kwa mwaka huo pia ilikuwa na GDP ya (62.41 Billion USD) yaani mara nne ya Pato la Taifa la Vietnam!Dah!

Labda ntaonekana naikandamiza Nchi yangu ya Tanzania,nirudi barani Afrika kidogo!Mwaka 1990 GDP ya Nchi ya Misri ilikuwa(42.98 Billion USD) wakati Nchi ya Tanzania tulikuwa na(4.259 Billion USD).Mpaka ninavyongea leo, GDP ya Nchi ya Misri ni mara sita ya GDP ya Nchi ya Tanzania kwa kuwa na (363.1 Billion USD).

Narudi kwa jirani mwema Nchini Kenya, yeye mwaka 1990 alikuwa na pato la Taifa la (8.572 Billion USD)karibia na sisi Tanzania lakini leo hii, Kenya ana Pato karibia mara mbili yetu la (98.84 billion USD)pamoja na kuwa na ukame wake wote,ukabila wake wote na umasikini wake wote wa rasilimali!Dah!

Wakati Nchi ya Nigeria ambayo utegemea madini ya mafuta tu kwa asilimia angalau 50, mpaka mwaka 2020 ilikuwa ni miongoni mwa Nchi zinazongoza kwa kuwa na pato la Taifa kubwa barani Afrika la kufikia (514.76 Billioni USD) wakati Tanzania imebarikiwa Gesi asilia,Tanzanite,Dhahabu,Almasi,Makaa ya mawe,Nickel,urenium au unaweza ukataja “jiwe” lolote ambalo halipo duniani lakini lipo Tanzania!Unaendaje kisherekea uhuru Taifa badala ya kutafuta majibu ya maswali haya!

Kiasi cha pato la Taifa la Nchi ya Nigeria(514.76 Billioni USD), kinatokana na sekta chache tu ambazo labda nizitaje hapa;sekta ya mafuta,sekta ya madini ya gesi,makaa ya mawe,metal ore,na mafuta ghafi labda niambie Tanzania haina kipi kati ya hivyo??

JE WATANZANIA TUNAPASWA KESHO TUJIPONGEZE AU TUENDELEE KUKUNA BONGO ZETU?

MH Hayati John Pombe Joseph Magufuli ni kama alikuwa anajua kuwa tumechezewa na tumechelewa sana na sio ajabu fedha ambayo inatumika kesho kuandaa sherehe za uhuru kwenye Nchi ambayo GDP yake ni mara nane ya GDP ya Nigeria,ingekuwa inaenda kwenye ujenzi wa Taifa na sio sherehe tena!

Nilitegemea sana fedha ambayo inaenda kutumika kesho pale uwanja wa Taifa kwa tukio la siku moja ingeenda kutumika katika kupambana na matatizo ya Watanzania kama ambayo Rais wangu Samia aliamua Ile fedha ya IMF & WB iende kujenga madarasa!

Wakati kaka yangu na kada mwenzangu Nape Nnauye, akitumia nguvu nyingi kuhoji mikopo iliyoifungua Nchi hii na kuiweka kwenye uchumi wa kati kabla ya muda wake yaani 2025 basi mtu huyu alipaswa atuambie tunatokaje hapa tulipo kwenye GDP ambayo haifanani na ukubwa wetu na heshima yetu kama Tanzania!Nani hajui kwamba sisi ni “political giant in Africa?”.

Nitoe somo kidogo kwa Watanzania wanaobeza miradi yetu ya kimkakati kwamba haina maana kwa Taifa hili!Eti SGR,Bwawa la Nyerere na Ndege zetu hazina maana!Khaa!

Nchi ya Malaysia ambayo ilianza mwaka 1963 tu mbele ya Tanzania ambayo ni mwaka 1961,leo hii ndio Nchi inayoogopwa barani Asia kwa Uchumi tishio na mkubwa!Mwaka 1990 GDP yake ilikuwa 43.370 Billion USD tu lakini mwaka 2015 ikawa ina GDP ya 247.539 Billion USD.

Nini kilitokea Nchini Malaysia mpaka wakafika hapo walipo?mambo makubwa matatu yanatajwa na historia ya Nchi hiyo katika kuwekeza kwenye kitu wanaita “Visible Projects” ambazo ni(I) Ujenzi wa uwanja mkubwa wa kimataifa wa ndege duniani yaani “Kuala Lumpur International Airport”,(II)Ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme yaani “Bakun Dam” na baadae (III)Ujenzi wa mradi mkubwa wa “multimedia Super Corridor”basi!

Unapata wapi “guards” za kuhoji mikopo ya awamu ya tano?kama ni International Airport ya JK Nyerere hiyo hapo,kama ni Bwawa la Umeme lile pale Rufiji na kama ni mkongo wa Taifa kwa ajili ya projects kama za Malaysia tunao!

Hivi tunakwama wapi Tanzania?hivi tunakosaje vichwa vichache”brains”za kumsaidia Mh Rais na Mama yangu hili tuweze kuipeleka mchakamchaka Nchi hii!Kesho ilipaswa kuwa siku nzuri ya kujitathimini kuliko kusherekea “uhuru” wetu huu!

SAA tatu usiku ya tarehe 8/12/2021 ndio hiyo inaelekea kufika,ngoja nisogee kwa TV nikamsikilize Rais WANGU na Mama yangu,Samia Suluhu Hassan,vijana tupo pamoja na Mama!

ULIPO MAMA NA SISI VIJANA TUPO”.

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Saut & Tumaini University Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %